Amosi 9:6 - Swahili Revised Union Version Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni, nayo dunia akaifunika kwa anga; huyaita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya nchi kavu. Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake! Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni, nayo dunia akaifunika kwa anga; huyaita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya nchi kavu. Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni, nayo dunia akaifunika kwa anga; huyaita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya nchi kavu. Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake! Neno: Bibilia Takatifu yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu na kuisimika misingi yake juu ya dunia, yeye aitaye maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi: Mwenyezi Mungu ndilo jina lake. Neno: Maandiko Matakatifu yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu na kuisimika misingi yake juu ya dunia, yeye aitaye maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: bwana ndilo jina lake. BIBLIA KISWAHILI Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake. |
Na kuziweka nguzo za ghorofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,
Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.
mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake;