Amosi 9:2 - Swahili Revised Union Version Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawateremsha toka huko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wajapojichimbia njia ya kwenda kuzimu, huko nitawachukua kwa mkono wangu; wajapopanda mbinguni, nitawaporomosha chini. Biblia Habari Njema - BHND Wajapojichimbia njia ya kwenda kuzimu, huko nitawachukua kwa mkono wangu; wajapopanda mbinguni, nitawaporomosha chini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wajapojichimbia njia ya kwenda kuzimu, huko nitawachukua kwa mkono wangu; wajapopanda mbinguni, nitawaporomosha chini. Neno: Bibilia Takatifu Wajapojichimbia chini hadi kwenye vina vya Kuzimu, kutoka huko mkono wangu utawatoa. Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu, kutoka huko nitawashusha. Neno: Maandiko Matakatifu Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu, kutoka huko mkono wangu utawatoa. Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu, kutoka huko nitawashusha. BIBLIA KISWAHILI Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawateremsha toka huko. |
Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.
ndipo nitakapokushusha pamoja nao washukao shimoni, uende kwa watu wa kale; nami nitakukalisha pande za chini za nchi; mahali palipokuwa ukiwa tangu zamani, pamoja nao washukao shimoni; ili usikaliwe na watu, wala usiweke utukufu wako katika nchi yao walio hai.
ili mti wowote, ulio karibu na maji, usijitukuze kwa sababu ya kimo chake, wala usitie kilele chake kati ya mawingu, wala mashujaa wake wasisimame katika kimo chao kirefu, naam, wote wanywao maji; maana wote wametolewa wafe, waende pande za chini za nchi, kati ya wanadamu, pamoja nao washukao shimoni.
Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kiota chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.