Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nitawaangamiza pamoja na dunia.
Amosi 8:2 - Swahili Revised Union Version Akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa joto. Ndipo BWANA akaniambia, Mwisho wao watu wangu Israeli umewajia; sitawapita tena kamwe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli. Sitavumilia tena maovu yao. Biblia Habari Njema - BHND Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli. Sitavumilia tena maovu yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli. Sitavumilia tena maovu yao. Neno: Bibilia Takatifu Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” Ndipo Mwenyezi Mungu akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.” Neno: Maandiko Matakatifu Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” Ndipo bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.” BIBLIA KISWAHILI Akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa joto. Ndipo BWANA akaniambia, Mwisho wao watu wangu Israeli umewajia; sitawapita tena kamwe. |
Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nitawaangamiza pamoja na dunia.
na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa joto, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake.
Na mimi, tazama, nitakaa Mizpa, ili nisimame mbele ya Wakaldayo watakaotujia; lakini ninyi chumeni divai, na matunda ya wakati wa jua, na mafuta, mkaviweke vitu hivyo katika vyombo vyenu, mkakae katika miji yenu mliyoitwaa.
Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?
Wanatuvizia hatua zetu, Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu; Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia; Maana mwisho wetu umefika.
Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Nitaikomesha mithali hii, wasiitumie tena kama mithali katika Israeli; lakini uwaambie, Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote.
Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitaleta upanga juu yako, nami nitakatilia mbali nawe wanadamu na wanyama.
Tena akaniambia, Mwanadamu, maneno yangu yote nitakayokuambia, yapokee moyoni mwako, na kuyasikia kwa masikio yako.
Bali nyumba ya Israeli hawatakusikiliza wewe; kwa kuwa hawanisikilizi mimi; maana nyumba yote ya Israeli wana vipaji vigumu, na mioyo yenye ukaidi.
Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii.
Basi, akaniambia, Umeyaona haya, Ee mwanadamu? Je! Ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye machukizo wanayoyafanya hapa? Kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha; na, tazama, wanaliweka tawi puani.
Akaniambia, Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, ili niende zangu mbali na patakatifu pangu? Lakini utaona tena machukizo makubwa mengine.
Siku za kupatilizwa zimekuja, siku za kulipa zimefika; Israeli atayajua hayo; huyo nabii ni mpumbavu, huyo mtu mwenye roho ana wazimu; kwa sababu ya wingi wa uovu wako, na kwa sababu uadui umekuwa mkubwa.
BWANA akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona timazi. Ndipo Bwana akasema, Tazama, nitaweka timazi kati ya watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe;
Ole wangu! Maana mimi ni kama hapo walipokwisha kuyachuma matunda ya wakati wa joto, kama zabibu zichumwazo baada ya mavuno; hapana shada la kuliwa; roho yangu inatamani tini iivayo kwanza.
Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la kitabu lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi.