Kwa kuwa BWANA atawapiga Israeli kama manyasi yatikiswavyo majini; naye atawang'oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng'ambo ya Mto; kwa sababu wamejitengenezea Maashera yao, wakimkasirisha BWANA.
Amosi 5:27 - Swahili Revised Union Version Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni, mwende mbali kupita Dameski, asema BWANA, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni, mbali kuliko Damasko! Hayo amesema Mwenyezi-Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa Majeshi. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni, mbali kuliko Damasko! Hayo amesema Mwenyezi-Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa Majeshi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni, mbali kuliko Damasko!” Hayo amesema Mwenyezi-Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa Majeshi. Neno: Bibilia Takatifu Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni mbali kupita Dameski,” asema Mwenyezi Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi ya mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni mbali kupita Dameski,” asema bwana, ambaye jina lake ni Mungu Mwenye Nguvu Zote. BIBLIA KISWAHILI Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni, mwende mbali kupita Dameski, asema BWANA, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi. |
Kwa kuwa BWANA atawapiga Israeli kama manyasi yatikiswavyo majini; naye atawang'oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng'ambo ya Mto; kwa sababu wamejitengenezea Maashera yao, wakimkasirisha BWANA.
Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
hata BWANA akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake, kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote, manabii. Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe, waende nchi ya Ashuru, hata leo.
Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.
Ndipo Yeremia akamwambia Sedekia, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama ukitoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi nafsi yako utaishi, wala mji huu hautateketezwa; nawe utaishi na nyumba yako;
Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.
Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyia wenyewe.
Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na hao wanaokaa salama katika mlima wa Samaria, watu mashuhuri wa taifa lililo la kwanza, ambao nyumba ya Israeli huwaendea.
Basi kwa ajili ya hayo sasa watakwenda utumwani pamoja na wa kwanza watakaokwenda utumwani, na kelele za shangwe za hao waliojinyosha zitakoma.
Nanyi mlichukua hema ya Moleki, Na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.