Amosi 4:2 - Swahili Revised Union Version Bwana MUNGU ameapa kwa utakatifu wake, ya kuwa, tazama, siku zitawajia, watakapowaondoa ninyi kwa kulabu, na mabaki yenu kwa ndoana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu Mtakatifu nimeapa: “Tazama, siku zaja, ambapo watu watawakokoteni kwa kulabu, kila mmoja wenu kama samaki kwenye ndoana. Biblia Habari Njema - BHND Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu Mtakatifu nimeapa: “Tazama, siku zaja, ambapo watu watawakokoteni kwa kulabu, kila mmoja wenu kama samaki kwenye ndoana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu Mtakatifu nimeapa: “Tazama, siku zaja, ambapo watu watawakokoteni kwa kulabu, kila mmoja wenu kama samaki kwenye ndoana. Neno: Bibilia Takatifu Bwana Mungu Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake: “Hakika wakati utakuja mtakapochukuliwa na kulabu, na wanaosalia kwa ndoana za samaki. Neno: Maandiko Matakatifu bwana Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake: “Hakika wakati utakuja mtakapochukuliwa na kulabu, na wanaosalia kwa ndoana za samaki. BIBLIA KISWAHILI Bwana MUNGU ameapa kwa utakatifu wake, ya kuwa, tazama, siku zitawajia, watakapowaondoa ninyi kwa kulabu, na mabaki yenu kwa ndoana. |
Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu, nitatia kulabu yangu katika pua yako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha kwa njia ile ile uliyoijia.
Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.
Nami nitatia kulabu katika taya zako, nami nitawashikamanisha samaki wa mito yako na magamba yako; nami nitakutoa katika mito yako, pamoja na samaki wa mito yako walioshikamana na magamba yako.
Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliotangatanga, nitawatibu waliojeruhiwa, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.
nami nitakugeuza na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;
Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.