Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao;
2 Wakorintho 3:4 - Swahili Revised Union Version Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tunaweza kusema hayo kwa sababu ya tumaini letu tulilo nalo kwa Mungu kwa njia ya Kristo. Biblia Habari Njema - BHND Tunaweza kusema hayo kwa sababu ya tumaini letu tulilo nalo kwa Mungu kwa njia ya Kristo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tunaweza kusema hayo kwa sababu ya tumaini letu tulilo nalo kwa Mungu kwa njia ya Kristo. Neno: Bibilia Takatifu Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kupitia kwa Al-Masihi. Neno: Maandiko Matakatifu Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Al-Masihi. BIBLIA KISWAHILI Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. |
Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao;
Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;
Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lolote.