Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoshika zamu siku ya sabato, mtalinda kasri ya mfalme;
2 Wafalme 11:7 - Swahili Revised Union Version Na sehemu mbili zenu, yaani, wote watokao siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya BWANA kumzunguka mfalme. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yale makundi mawili ambayo humaliza zamu yao siku ya Sabato yatashika zamu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kumlinda mfalme. Biblia Habari Njema - BHND Yale makundi mawili ambayo humaliza zamu yao siku ya Sabato yatashika zamu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kumlinda mfalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yale makundi mawili ambayo humaliza zamu yao siku ya Sabato yatashika zamu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kumlinda mfalme. Neno: Bibilia Takatifu Nanyi ambao mko katika makundi mengine mawili ambao kwa kawaida hupumzika siku ya Sabato, wote mtalinda Hekalu kwa ajili ya mfalme. Neno: Maandiko Matakatifu nanyi ambao mko katika makundi mengine mawili ambao kwa kawaida hupumzika Sabato, wote mtalinda Hekalu kwa ajili ya mfalme. BIBLIA KISWAHILI Na sehemu mbili zenu, yaani, wote watokao siku ya sabato, mtashika zamu za ulinzi katika nyumba ya BWANA kumzunguka mfalme. |
Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoshika zamu siku ya sabato, mtalinda kasri ya mfalme;
na theluthi mtakuwapo mlangoni pa Suri; na theluthi langoni nyuma ya walinzi; hivyo ndivyo mtalinda kasri, kuzuia watu wasiingie.
Mtamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake mkononi; naye awaye yote aingiaye ndani ya safu auawe; mkafuatane na mfalme, akitoka na akiingia.
Na ndugu zao, katika vijiji vyao, wakawajibika kuingia kila siku ya saba, zamu kwa zamu, ili kuwa pamoja nao;
Wala asiingie mtu nyumbani mwa BWANA, ila makuhani, na Walawi watumikao; hao wataingia, kwa kuwa ni watakatifu; ila watu wengine wote watafuata amri za BWANA.