Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 11:5 - Swahili Revised Union Version

5 Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoshika zamu siku ya sabato, mtalinda kasri ya mfalme;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kisha akatoa amri: “Mtafanya hivi: Mtakapokuja kushika zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda ikulu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kisha akatoa amri: “Mtafanya hivi: Mtakapokuja kushika zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda ikulu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kisha akatoa amri: “Mtafanya hivi: mtakapokuja kushika zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda ikulu;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaoingia zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda jumba la kifalme,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaoingia zamu siku ya Sabato, theluthi yenu inayolinda jumba la kifalme,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoshika zamu siku ya sabato, mtalinda nyumba ya mfalme;

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 11:5
12 Marejeleo ya Msalaba  

na chakula cha mezani pake, na maofisa wake walivyokaa, na kuhudumu kwao wahudumu wake, na mavazi yao, na wanyweshaji wake, na sadaka zake za kuteketezwa ambazo alizitoa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.


Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa BWANA, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme.


na theluthi mtakuwapo mlangoni pa Suri; na theluthi langoni nyuma ya walinzi; hivyo ndivyo mtalinda kasri, kuzuia watu wasiingie.


Na ukumbi wa sabato walioujenga katika hiyo nyumba, na mahali pa kuingia pake mfalme palipokuwapo nje, akavigeuza kuikabili nyumba ya BWANA, kwa sababu ya mfalme wa Ashuru.


tena ni wajibu wao kuitunza hema ya kukutania na patakatifu na kuwasaidia wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya BWANA.


Na ndugu zao, katika vijiji vyao, wakawajibika kuingia kila siku ya saba, zamu kwa zamu, ili kuwa pamoja nao;


Na wakuu wa Yuda waliposikia habari za mambo haya, wakatoka katika nyumba ya mfalme, wakapanda juu mpaka nyumbani kwa BWANA; wakaketi, hapo watu waingiliapo katika lango jipya la nyumba ya BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo