Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao tumboni, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri.
2 Samueli 20:20 - Swahili Revised Union Version Yoabu akajibu, akasema, Isiwe, isiwe kwangu, niumeze wala kuuharibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yoabu akamjibu, “Kamwe maishani mwangu! Sina nia kuangamiza wala kuharibu. Biblia Habari Njema - BHND Yoabu akamjibu, “Kamwe maishani mwangu! Sina nia kuangamiza wala kuharibu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yoabu akamjibu, “Kamwe maishani mwangu! Sina nia kuangamiza wala kuharibu. Neno: Bibilia Takatifu Yoabu akajibu, “Hilo liwe mbali nami. Hilo liwe mbali nami kumeza au kuharibu. Neno: Maandiko Matakatifu Yoabu akajibu, “Hilo liwe mbali nami. Hilo liwe mbali nami kumeza au kuharibu. BIBLIA KISWAHILI Yoabu akajibu, akasema, Isiwe, isiwe kwangu, niumeze wala kuuharibu. |
Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao tumboni, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri.
Mimi ni mmoja wa hao wenye amani, walio waaminifu katika Israeli; wewe unataka kuuharibu mji ulio kama mama wa Israeli; mbona unataka kuumeza urithi wa BWANA?
Neno hili silo hivyo; lakini mtu mmoja wa milima ya Efraimu, jina lake, Sheba, mwana wa Bikri, ameinua mkono wake juu ya mfalme, naam, Daudi, basi mtoeni yeye tu, nami nitaondoka katika mji huu. Basi yule mwanamke akamwambia Yoabu, Tazama, kichwa chake utatupiwa juu ya ukuta.
Akasema, Hasha, BWANA, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatarisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.
Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema; Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.