Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
2 Samueli 17:7 - Swahili Revised Union Version Hushai akamwambia Absalomu, Ushauri huu alioutoa Ahithofeli si mwema wakati huu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hushai akamwambia Absalomu, “Wakati huu, shauri alilolitoa Ahithofeli si jema.” Biblia Habari Njema - BHND Hushai akamwambia Absalomu, “Wakati huu, shauri alilolitoa Ahithofeli si jema.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hushai akamwambia Absalomu, “Wakati huu, shauri alilolitoa Ahithofeli si jema.” Neno: Bibilia Takatifu Hushai akamjibu Absalomu, “Ushauri alioutoa Ahithofeli haufai kwa wakati huu. Neno: Maandiko Matakatifu Hushai akamjibu Absalomu, “Shauri la Ahithofeli alilotoa halifai kwa wakati huu. BIBLIA KISWAHILI Hushai akamwambia Absalomu, Ushauri huu alioutoa Ahithofeli si mwema wakati huu. |
Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
lakini ukirudi mjini, na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tokea zamani, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako sasa; ndipo utayavunja mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.
Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria wa baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe.
Basi Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu akamwambia, akasema, Ahithofeli amesema hivi; je! Tufanye kama alivyosema? Kama sivyo, sema maneno yako.