Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri.
2 Samueli 13:14 - Swahili Revised Union Version Lakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamlazimisha, akalala naye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Amnoni hakutaka kumsikiliza na kwa kuwa alimzidi nguvu, alimlazimisha, akalala naye. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Amnoni hakutaka kumsikiliza na kwa kuwa alimzidi nguvu, alimlazimisha, akalala naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Amnoni hakutaka kumsikiliza na kwa kuwa alimzidi nguvu, alimlazimisha, akalala naye. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Amnoni akakataa kumsikiliza, na kwa kuwa alikuwa na nguvu kuliko Tamari, akamtenda jeuri. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Amnoni akakataa kumsikiliza, na kwa kuwa alikuwa na nguvu kuliko Tamari, akamtenda jeuri. BIBLIA KISWAHILI Lakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamlazimisha, akalala naye. |
Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri.
BWANA asema hivi, Angalia, nitakuzushia uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako hadharani.
Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako.
Kisha mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ngome hadi mahali pa karamu ya divai. Ikawa Hamani amejitupa chini penye kitanda alipokuwapo Esta. Mfalme akasema, Namna gani! Je! Atamfanyia malkia jeuri hata machoni pangu nyumbani mwangu? Na neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, wakamfunika uso Hamani.
Utupu wa dada yako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe alizaliwa nyumbani mwenu au kwingine, utupu wa hao usifunue.
Na alaaniwe alalaye na dada yake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.
Nao wanaume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walitaka kuniua, na suria wangu wakambaka nguvu, hata amekufa.