Akawauliza, Je! Hajambo? Wakasema, Hajambo; tazama, Raheli binti yake anakuja na kondoo.
2 Samueli 11:7 - Swahili Revised Union Version Uria alipomwendea Daudi, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, na habari za watu, na habari za vita. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uria alipofika kwake, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, watu wote, na hali ya vita. Biblia Habari Njema - BHND Uria alipofika kwake, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, watu wote, na hali ya vita. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uria alipofika kwake, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, watu wote, na hali ya vita. Neno: Bibilia Takatifu Uria alipofika, Daudi akamuuliza habari za Yoabu, hali za askari na vita kwamba inaendeleaje. Neno: Maandiko Matakatifu Uria alipofika, Daudi akamuuliza habari za Yoabu, hali za askari na vita kwamba inaendeleaje. BIBLIA KISWAHILI Uria alipomwendea Daudi, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, na habari za watu, na habari za vita. |
Akawauliza, Je! Hajambo? Wakasema, Hajambo; tazama, Raheli binti yake anakuja na kondoo.
Akamwambia, Nenda, basi, ukaone kama ndugu zako hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akamtuma kutoka bonde la Hebroni, na akafika Shekemu.
Ndipo Daudi akapeleka habari kwa Yoabu, akisema, Mtume kwangu Uria, Mhiti. Naye Yoabu akamtuma Uria kwa Daudi.
Basi Musa akatoka nje ili amlaki mkwewe, akasujudia na kumbusu; nao wakaulizana habari; kisha wakaingia hemani.
Basi Daudi akaviacha vile vyombo vyake katika mkono wa mlinda vyombo, akalikimbilia jeshi, akafika, akawasalimu ndugu zake.