Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.
2 Samueli 1:24 - Swahili Revised Union Version Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wanawake wa Israeli, mlilieni Shauli! Aliwavika mavazi mekundu ya fahari, aliyatarizi mavazi yenu kwa dhahabu. Biblia Habari Njema - BHND “Wanawake wa Israeli, mlilieni Shauli! Aliwavika mavazi mekundu ya fahari, aliyatarizi mavazi yenu kwa dhahabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Wanawake wa Israeli, mlilieni Shauli! Aliwavika mavazi mekundu ya fahari, aliyatarizi mavazi yenu kwa dhahabu. Neno: Bibilia Takatifu “Enyi binti za Israeli, lieni kwa ajili ya Sauli, ambaye aliwavika nguo nyekundu na maridadi, ambaye alirembesha mavazi yenu kwa mapambo ya dhahabu. Neno: Maandiko Matakatifu “Enyi binti za Israeli, lieni kwa ajili ya Sauli, ambaye aliwavika nguo nyekundu na maridadi, ambaye aliremba mavazi yenu kwa mapambo ya dhahabu. BIBLIA KISWAHILI Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu. |
Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.
Jinsi mashujaa walivyoanguka Katikati ya vita! Ee Yonathani, wewe umeuawa Juu ya mahali pako palipoinuka.
Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu.
Je! Hawakupata mateka na kuyagawanya, Kijakazi, vijakazi wawili, kwa kila mtu? Kwa Sisera nyara ya mavazi ya rangi mbalimbali, Nyara za mavazi ya rangi mbalimbali ya darizi; Ya rangi mbalimbali ya darizi, pande zote mbili, Juu ya shingo za hao mateka.