1 Yohana 4:8 - Swahili Revised Union Version Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo. Biblia Habari Njema - BHND Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo. Neno: Bibilia Takatifu Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mwenyezi Mungu ni pendo. BIBLIA KISWAHILI Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. |
Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lolote hamna ndani yake.
Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.
Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.