1 Wakorintho 10:8 - Swahili Revised Union Version Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu elfu ishirini na tatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000. Biblia Habari Njema - BHND Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000. Neno: Bibilia Takatifu Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu elfu ishirini na tatu kwa siku moja. Neno: Maandiko Matakatifu Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. BIBLIA KISWAHILI Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu elfu ishirini na tatu. |
lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie kikwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.