1 Wafalme 8:12 - Swahili Revised Union Version Ndipo Sulemani akanena, BWANA alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo Solomoni akasema, “Mwenyezi-Mungu alisema kwamba, atakaa katika giza nene. Biblia Habari Njema - BHND Ndipo Solomoni akasema, “Mwenyezi-Mungu alisema kwamba, atakaa katika giza nene. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo Solomoni akasema, “Mwenyezi-Mungu alisema kwamba, atakaa katika giza nene. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Sulemani akasema, “Mwenyezi Mungu alisema kwamba ataishi katika giza nene; Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Sulemani akasema, “bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene; BIBLIA KISWAHILI Ndipo Sulemani akanena, BWANA alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. |
hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya BWANA ilikuwa imejaa utukufu wa BWANA.
Ezra akakifunua kitabu machoni pa watu wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote walisimama;
BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wowote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema.
Mkakaribia, mkasimama chini ya ule mlima; mlima ukawaka moto mpaka kati ya mbinguni, kwa giza na mawingu, na giza kuu.
Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.
Maana hamkufikia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,