Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




1 Wafalme 8:10 - Swahili Revised Union Version

Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya BWANA ikajaa wingu;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ikawa, makuhani walipotoka pale mahali patakatifu, wingu liliijaza nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ikawa, makuhani walipotoka pale mahali patakatifu, wingu liliijaza nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ikawa, makuhani walipotoka pale mahali patakatifu, wingu liliijaza nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la bwana.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya BWANA ikajaa wingu;

Tazama sura
Tafsiri zingine



1 Wafalme 8:10
11 Marejeleo ya Msalaba  

hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya BWANA ilikuwa imejaa utukufu wa BWANA.


Mawingu na giza vyamzunguka, Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.


Ilikuwa Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli, wakaangalia upande wa bara, na tazama, utukufu wa BWANA ukaonekana katika hilo wingu.


Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.


Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.


Utukufu wa BWANA ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba; nayo nyumba ikajazwa na lile wingu, na ua ulikuwa umejaa mwangaza wa utukufu wa BWANA.


BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wowote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema.


nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema BWANA wa majeshi.


Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, mpaka yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.