Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya jina la BWANA, alikuja ili amjaribu kwa maswali ya fumbo.
1 Wafalme 4:34 - Swahili Revised Union Version Watu wakaja kutoka mataifa yote, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake, ili waisikie hekima ya Sulemani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu kutoka mataifa yote, na wafalme wote waliopata kusikia habari kuhusu hekima yake, walikuja kumsikiliza. Biblia Habari Njema - BHND Watu kutoka mataifa yote, na wafalme wote waliopata kusikia habari kuhusu hekima yake, walikuja kumsikiliza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu kutoka mataifa yote, na wafalme wote waliopata kusikia habari kuhusu hekima yake, walikuja kumsikiliza. Neno: Bibilia Takatifu Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Sulemani, wakiwa wametumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia kuhusu hekima yake. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Sulemani, waliotumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia juu ya hekima yake. BIBLIA KISWAHILI Watu wakaja kutoka mataifa yote, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake, ili waisikie hekima ya Sulemani. |
Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya jina la BWANA, alikuja ili amjaribu kwa maswali ya fumbo.
Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.
Na malkia wa Sheba aliposikia sifa za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, akiwa na wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Wafalme wote wa duniani wakamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni.
Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.
BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yuko pamoja nanyi.