Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la Agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.
1 Wafalme 3:16 - Swahili Revised Union Version Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku moja, wanawake wawili makahaba, walikwenda kwa mfalme Solomoni. Biblia Habari Njema - BHND Siku moja, wanawake wawili makahaba, walikwenda kwa mfalme Solomoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku moja, wanawake wawili makahaba, walikwenda kwa mfalme Solomoni. Neno: Bibilia Takatifu Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake. Neno: Maandiko Matakatifu Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake. BIBLIA KISWAHILI Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake. |
Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la Agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.
Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nilizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani.
Asubuhi yake Musa akaketi ili awapishie hukumu watu; na hao watu wakasimama kumzunguka Musa tangu asubuhi hata jioni.
wakiwa na neno, hunijia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajulisha amri za Mungu, na sheria zake.
Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu.
Nao wakasimama mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya wakuu, na mkutano wote, mlangoni pa hema ya kukutania, wakasema,
Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.
Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Nendeni mkaitazame nchi hii, hasa Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha.