Ndipo mfalme wa Israeli, akawaita wazee wote wa nchi, akasema, Angalieni, nawaomba, mwone, kwamba huyu ataka madhara; maana ametuma kwangu kutaka wake zangu na watoto wangu; na fedha yangu na dhahabu yangu, sikumkatalia.
1 Wafalme 20:8 - Swahili Revised Union Version Wakamwambia wazee wote na watu wote, Usisikie, wala usikubali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wazee na watu wote wakamwambia, “Usimjali wala usikubali.” Biblia Habari Njema - BHND Wazee na watu wote wakamwambia, “Usimjali wala usikubali.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wazee na watu wote wakamwambia, “Usimjali wala usikubali.” Neno: Bibilia Takatifu Wazee na watu wote wakajibu, “Usimsikilize, wala usiyakubali matakwa yake.” Neno: Maandiko Matakatifu Wazee na watu wote wakajibu, “Usimsikilize, wala usiyakubali matakwa yake.” BIBLIA KISWAHILI Wakamwambia wazee wote na watu wote, Usisikie, wala usikubali. |
Ndipo mfalme wa Israeli, akawaita wazee wote wa nchi, akasema, Angalieni, nawaomba, mwone, kwamba huyu ataka madhara; maana ametuma kwangu kutaka wake zangu na watoto wangu; na fedha yangu na dhahabu yangu, sikumkatalia.
Kwa hiyo akawaambia wale wajumbe wa Ben-hadadi, Mwambieni bwana wangu mfalme, Kila uliyotuma kumtakia mtumwa wako kwanza, nitafanya, ila neno hili siwezi kulifanya. Basi wajumbe wakaenda zao, wakamrudishia maneno hayo.