Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya BWANA, akaukunjua mbele za BWANA.
1 Samueli 8:21 - Swahili Revised Union Version Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Samueli alipokwisha sikiliza kila kitu walichosema, akaenda na kumweleza Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Samueli alipokwisha sikiliza kila kitu walichosema, akaenda na kumweleza Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Samueli alipokwisha sikiliza kila kitu walichosema, akaenda na kumweleza Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Samweli aliposikia yote watu waliyosema, akarudia kuyasema mbele za Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Samweli aliposikia yote watu waliyosema, akarudia kuyasema mbele za bwana. BIBLIA KISWAHILI Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa BWANA. |
Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya BWANA, akaukunjua mbele za BWANA.
Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kiongozi, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya BWANA huko Mispa.
BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawateulie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Kila mtu aende nyumbani kwake.