Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Samueli 5:9 - Swahili Revised Union Version

Ikawa, walipolihamisha, mkono wa BWANA ulikuwa juu ya mji huo, kwa kuwafadhaisha sana; akawapiga watu wa mjini, wadogo kwa wakubwa, wakapatwa na majipu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lakini baada ya kulipeleka huko Gathi, Mwenyezi-Mungu akauadhibu mji huo, akisababisha hofu kuu mjini, na akawapiga wanaume wa mji huo, vijana kwa wazee, kwa kuwaletea majipu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lakini baada ya kulipeleka huko Gathi, Mwenyezi-Mungu akauadhibu mji huo, akisababisha hofu kuu mjini, na akawapiga wanaume wa mji huo, vijana kwa wazee, kwa kuwaletea majipu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lakini baada ya kulipeleka huko Gathi, Mwenyezi-Mungu akauadhibu mji huo, akisababisha hofu kuu mjini, na akawapiga wanaume wa mji huo, vijana kwa wazee, kwa kuwaletea majipu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Lakini baada ya kulihamisha, mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa dhidi ya huo mji wa Gathi, akiuweka katika fadhaa kuu. Mungu akawatesa watu wa huo mji, vijana kwa wazee, kwa kuwaletea majipu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Lakini baada ya kulihamisha, mkono wa bwana ulikuwa dhidi ya huo mji wa Gathi, akiuweka katika fadhaa kuu. Mungu akawatesa watu wa huo mji, vijana kwa wazee, kwa kuwaletea majipu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ikawa, walipolihamisha, mkono wa BWANA ulikuwa juu ya mji huo, kwa kuwafadhaisha sana; akawapiga watu wa mjini, wadogo kwa wakubwa, wakapatwa na majipu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Samueli 5:9
11 Marejeleo ya Msalaba  

Akawapiga watesi wake akawarudisha nyuma, Akawatia aibu ya milele.

Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.

Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa katika kambi hadi walipouwawa.

Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu.

Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu mpaka Ekroni. Ikawa, sanduku la Mungu lilipofika Ekroni, watu wa Ekroni walipiga kelele, wakasema, Wamelileta hilo sanduku la Mungu wa Israeli kwetu, ili kutuua sisi na watu wetu.

Kwa hiyo wakatuma watu waende kuwakusanya wakuu wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake, ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini kote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.

Lakini mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaangamiza, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake.

kisha wakaliweka sanduku la BWANA juu ya gari, pamoja na kasha lenye panya wa dhahabu na sanamu za majipu yao.

Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli.