Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
1 Samueli 26:4 - Swahili Revised Union Version Basi Daudi akatuma wapelelezi, akapata habari ya hakika ya kwamba Sauli amefika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema alituma wapelelezi, akafahamishwa kwamba ni kweli. Biblia Habari Njema - BHND alituma wapelelezi, akafahamishwa kwamba ni kweli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza alituma wapelelezi, akafahamishwa kwamba ni kweli. Neno: Bibilia Takatifu Daudi akatuma wapelelezi na akapata habari kwa hakika kwamba Sauli alikuwa amewasili. Neno: Maandiko Matakatifu Daudi akatuma wapelelezi na akapata habari kwa hakika kwamba Sauli alikuwa amewasili. BIBLIA KISWAHILI Basi Daudi akatuma wapelelezi, akapata habari ya hakika ya kwamba Sauli amefika. |
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Nendeni mkaitazame nchi hii, hasa Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
Naye Sauli akapiga hema katika kilima cha Hakila, kilichoelekea Yeshimoni, barabarani; lakini Daudi alikuwa akikaa nyikani, akaona ya kwamba Sauli amemfuata mpaka nyikani.
Daudi akainuka, akafika mahali pale alipotua Sauli; Daudi akapaangalia mahali alipolala Sauli, na Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi lake; naye Sauli alikuwa amelala kati ya magari, na hao watu wamepiga hema zao wakimzunguka.