Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha BWANA kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli.
1 Samueli 23:18 - Swahili Revised Union Version Na hao wawili wakafanya agano mbele za BWANA; Daudi naye akakaa huko Horeshi, na Yonathani akaenda nyumbani kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao wote wawili, wakafanya agano mbele ya Mwenyezi-Mungu. Daudi akabaki mjini Horeshi na Yonathani akaenda zake nyumbani. Biblia Habari Njema - BHND Hao wote wawili, wakafanya agano mbele ya Mwenyezi-Mungu. Daudi akabaki mjini Horeshi na Yonathani akaenda zake nyumbani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao wote wawili, wakafanya agano mbele ya Mwenyezi-Mungu. Daudi akabaki mjini Horeshi na Yonathani akaenda zake nyumbani. Neno: Bibilia Takatifu Wote wawili wakafanya agano mbele za Mwenyezi Mungu. Kisha Yonathani akaenda zake nyumbani, lakini Daudi akabaki Horeshi. Neno: Maandiko Matakatifu Wote wawili wakaweka agano mbele za bwana. Kisha Yonathani akaenda zake nyumbani, lakini Daudi akabaki Horeshi. BIBLIA KISWAHILI Na hao wawili wakafanya agano mbele za BWANA; Daudi naye akakaa huko Horeshi, na Yonathani akaenda nyumbani kwake. |
Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha BWANA kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli.
Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani?
Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.
Naye Yonathani akamwambia Daudi, Nenda kwa amani; kwa maana sisi sote wawili tumeapiana kwa jina la BWANA ya kwamba, BWANA atakuwa kati ya mimi na wewe, na kati ya uzao wangu na uzao wako milele. Daudi akaondoka, akaenda zake; Yonathani naye akaenda zake mjini.
Basi, unitendee mema mimi mtumishi wako; kwa sababu umenitia mimi mtumishi wako katika agano la BWANA pamoja nawe, lakini ikiwa mna uovu moyoni mwangu, uniue wewe mwenyewe; kwa nini kunileta kwa baba yako?
Basi Daudi akaenda Nobu kwa Ahimeleki, kuhani. Ahimeleki akaenda kumlaki Daudi, akitetemeka, akamwambia, Kwa nini uko peke yako, wala hapana mtu pamoja nawe?