Mtu atakapomshika ndugu yake ndani ya nyumba ya baba yake, akisema, Wewe una nguo, ututawale wewe; na mahali hapa palipobomoka pawe chini ya mkono wako;
1 Samueli 21:3 - Swahili Revised Union Version Kuna nini basi, chini ya mkono wako? Nipe mkononi mwangu mikate mitano, au chochote ulicho nacho hapa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, una kitu chochote? Nakuomba mikate mitano au chochote kilichoko.” Biblia Habari Njema - BHND Je, una kitu chochote? Nakuomba mikate mitano au chochote kilichoko.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, una kitu chochote? Nakuomba mikate mitano au chochote kilichoko.” Neno: Bibilia Takatifu Sasa basi, una nini mkononi? Nipatie mikate mitano au chochote unachoweza kupata.” Neno: Maandiko Matakatifu Sasa basi, una nini mkononi? Nipatie mikate mitano au chochote unachoweza kupata.” BIBLIA KISWAHILI Kuna nini basi, chini ya mkono wako? Nipe mkononi mwangu mikate mitano, au chochote ulicho nacho hapa. |
Mtu atakapomshika ndugu yake ndani ya nyumba ya baba yake, akisema, Wewe una nguo, ututawale wewe; na mahali hapa palipobomoka pawe chini ya mkono wako;
Laiti watu hawa wangekuwa chini ya mkono wangu! Hapo basi mimi ningemuondoa huyo Abimeleki. Kisha akamwambia Abimeleki, Haya, ongeza jeshi lako, utokeze.
Daudi akamwambia Ahimeleki, kuhani, Mfalme ameniagiza shughuli, akaniambia, Asijue mtu awaye yote habari ya shughuli hii ninayokutuma, wala ya neno hili ninalokuamuru; nami nimewaagiza vijana waende mahali fulani.
Yule kuhani akamjibu Daudi, akasema, Hapana mikate ya kawaida chini ya mkono wangu, ila mikate mitakatifu; ikiwa wale vijana wamejitenga na wanawake.