1 Samueli 2:19 - Swahili Revised Union Version Tena mamaye alimshonea kanzu ndogo, na kumletea kila mwaka, hapo alipokwea pamoja na mumewe ili kutoa dhabihu kila mwaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila mwaka mama yake alimfumia vazi dogo, na kumpelekea alipokuwa akienda na mumewe kutolea tambiko ya kila mwaka. Biblia Habari Njema - BHND Kila mwaka mama yake alimfumia vazi dogo, na kumpelekea alipokuwa akienda na mumewe kutolea tambiko ya kila mwaka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila mwaka mama yake alimfumia vazi dogo, na kumpelekea alipokuwa akienda na mumewe kutolea tambiko ya kila mwaka. Neno: Bibilia Takatifu Kila mwaka mama yake alimshonea joho dogo na kumpelekea alipokwea pamoja na mumewe kutoa dhabihu ya mwaka. Neno: Maandiko Matakatifu Kila mwaka mama yake alimshonea joho dogo na kumchukulia wakati alipokwea pamoja na mumewe kutoa dhabihu ya mwaka. BIBLIA KISWAHILI Tena mamaye alimshonea kanzu ndogo, na kumletea kila mwaka, hapo alipokwea pamoja na mumewe ili kutoa dhabihu kila mwaka. |
Kisha yule mtu, Elkana, na watu wote wa nyumbani mwake, wakakwea kwenda kumtolea BWANA dhabihu ya mwaka, na nadhiri yake.
Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.