1 Samueli 19:19 - Swahili Revised Union Version Naye Sauli akaambiwa, Angalia, yule Daudi yuko katika Nayothi, huko Rama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baadaye Shauli aliambiwa kuwa Daudi alikuwa huko Nayothi katika Rama. Biblia Habari Njema - BHND Baadaye Shauli aliambiwa kuwa Daudi alikuwa huko Nayothi katika Rama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baadaye Shauli aliambiwa kuwa Daudi alikuwa huko Nayothi katika Rama. Neno: Bibilia Takatifu Habari zikamfikia Sauli kusema: “Daudi yuko Nayothi huko Rama.” Neno: Maandiko Matakatifu Habari zikamfikia Sauli kusema: “Daudi yuko Nayothi huko Rama.” BIBLIA KISWAHILI Naye Sauli akaambiwa, Angalia, yule Daudi yuko katika Nayothi, huko Rama. |
Hivyo Daudi akakimbia, akajiponya, akamwendea Samweli huko Rama, akamwambia hayo yote Sauli aliyomtenda. Kisha yeye na Samweli wakaenda na kukaa katika Nayothi.
Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, Roho ya Mungu ikawajia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.
Ndipo wale Wazifi wakakwea kwa Sauli huko Gibea, wakasema, Je! Yule Daudi hakujificha kwetu ngomeni mwa Horeshi, kilimani pa Hakila upande wa kusini wa Yeshimoni?
Basi hao Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea, wakasema, Je! Yule Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kuelekea Yeshimoni?