Nao watumishi wa Absalomu wakamwendea yule mwanamke mle nyumbani; wakasema, Wako wapi Yonathani na Ahimaasi? Yule mwanamke akawaambia, Wamevuka kijito cha maji. Basi walipokwisha kuwatafuta wasiwaone, wakarudi Yerusalemu.
1 Samueli 19:14 - Swahili Revised Union Version Naye Sauli alipotuma wajumbe ili kumkamata Daudi, yeye alisema, Mgonjwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shauli alipotuma watu kumshika Daudi, Mikali akawaambia kuwa Daudi ni mgonjwa. Biblia Habari Njema - BHND Shauli alipotuma watu kumshika Daudi, Mikali akawaambia kuwa Daudi ni mgonjwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shauli alipotuma watu kumshika Daudi, Mikali akawaambia kuwa Daudi ni mgonjwa. Neno: Bibilia Takatifu Sauli alipotuma watu kumkamata Daudi, Mikali akasema, “Yeye ni mgonjwa.” Neno: Maandiko Matakatifu Sauli alipotuma watu kumkamata Daudi, Mikali akasema, “Yeye ni mgonjwa.” BIBLIA KISWAHILI Naye Sauli alipotuma wajumbe ili kumkamata Daudi, yeye alisema, Mgonjwa. |
Nao watumishi wa Absalomu wakamwendea yule mwanamke mle nyumbani; wakasema, Wako wapi Yonathani na Ahimaasi? Yule mwanamke akawaambia, Wamevuka kijito cha maji. Basi walipokwisha kuwatafuta wasiwaone, wakarudi Yerusalemu.
ikawa kama wakati wa kufungwa lango la mji, kulipokuwa giza, watu wale wakatoka, wala sijui walikokwenda; wafuateni upesi, maana mtawapata.
Basi Sauli akawatuma hao wajumbe ili wamtazame Daudi, akisema, Mleteni kwangu juu ya kitanda chake, nipate kumwua.
Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, Roho ya Mungu ikawajia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.