Nao watumishi wa Absalomu wakamwendea yule mwanamke mle nyumbani; wakasema, Wako wapi Yonathani na Ahimaasi? Yule mwanamke akawaambia, Wamevuka kijito cha maji. Basi walipokwisha kuwatafuta wasiwaone, wakarudi Yerusalemu.
1 Samueli 19:12 - Swahili Revised Union Version Basi Mikali akamteremsha Daudi dirishani; naye akaenda akakimbia na kuokoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akatoka na kutoroka. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akatoka na kutoroka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akatoka na kutoroka. Neno: Bibilia Takatifu Basi Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akakimbia na kuokoka. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akakimbia na kuokoka. BIBLIA KISWAHILI Basi Mikali akamteremsha Daudi dirishani; naye akaenda akakimbia na kuokoka. |
Nao watumishi wa Absalomu wakamwendea yule mwanamke mle nyumbani; wakasema, Wako wapi Yonathani na Ahimaasi? Yule mwanamke akawaambia, Wamevuka kijito cha maji. Basi walipokwisha kuwatafuta wasiwaone, wakarudi Yerusalemu.
Ndipo akawashusha kwa kamba dirishani, maana nyumba yake ilikuwa katika ukuta wa mji; naye alikaa ukutani.
Basi, wana wa Sauli walikuwa ni hawa, Yonathani, na Ishvi, na Malkishua; na majina ya binti zake wawili yalikuwa haya; jina lake wa kwanza aliitwa Merabu, na jina lake mdogo aliitwa Mikali;