Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
1 Samueli 17:24 - Swahili Revised Union Version Na watu wote wa Israeli walipomwona yule mtu wakakimbia, wakaogopa sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli walipomwona Goliathi, walimkimbia, na kumwogopa sana. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli walipomwona Goliathi, walimkimbia, na kumwogopa sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waisraeli walipomwona Goliathi, walimkimbia, na kumwogopa sana. Neno: Bibilia Takatifu Waisraeli walipomwona yule mtu, wote wakamkimbia kwa woga mkuu. Neno: Maandiko Matakatifu Waisraeli walipomwona yule mtu, wote wakamkimbia kwa woga mkuu. BIBLIA KISWAHILI Na watu wote wa Israeli walipomwona yule mtu wakakimbia, wakaogopa sana. |
Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
Kisha watu wa nyumba ya Daudi wakaambiwa kwamba Shamu wamefanya mapatano na Efraimu. Na moyo wake ukataharuki, na moyo wa watu wake, kama miti ya mwituni itikiswavyo na upepo.
Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye.
Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa?
Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana.
Hata alipokuwa akisema nao, kumbe! Yule shujaa alitokea, yule Mfilisti wa Gathi, jina lake Goliathi, akitoka katika jeshi la Wafilisti, akasema maneno yale yale; naye Daudi akayasikia.
Watu wa Israeli wakasema, Je! Mmemwona mtu huyu aliyepanda huko? Hakika ametokea ili awatukane Israeli; basi, itakuwa, mtu yule atakayemwua, mfalme atampa utajiri mwingi, naye atamwoza binti yake, na kuufanya ukoo wa baba yake kuwa huru katika Israeli.