Kisha akatwaa watu kama elfu tano, akawaweka kuotea kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa huo mji.
1 Samueli 15:5 - Swahili Revised Union Version Sauli akaufikia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Halafu yeye na watu wake wakaenda kwenye mji wa Amaleki, wakawa wakivizia kwenye bonde. Biblia Habari Njema - BHND Halafu yeye na watu wake wakaenda kwenye mji wa Amaleki, wakawa wakivizia kwenye bonde. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Halafu yeye na watu wake wakaenda kwenye mji wa Amaleki, wakawa wakivizia kwenye bonde. Neno: Bibilia Takatifu Sauli akaenda katika mji wa Amaleki na kuwavizia bondeni. Neno: Maandiko Matakatifu Sauli akaenda katika mji wa Amaleki na kuwavizia bondeni. BIBLIA KISWAHILI Sauli akaufikia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. |
Kisha akatwaa watu kama elfu tano, akawaweka kuotea kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa huo mji.
Akawaagiza, akasema, Angalieni, mtaotea kuuvizia ule mji, upande wa nyuma wa mji; msiende mbali sana na mji, lakini kaeni tayari nyote;
Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari wa miguu elfu mia mbili na watu elfu kumi wa Yuda.
Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Nendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki.