1 Samueli 15:14 - Swahili Revised Union Version Samweli akasema, Maana yake nini basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Samueli akamwambia, “Mbona nasikia mlio wa kondoo na ng'ombe?” Biblia Habari Njema - BHND Samueli akamwambia, “Mbona nasikia mlio wa kondoo na ng'ombe?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Samueli akamwambia, “Mbona nasikia mlio wa kondoo na ng'ombe?” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Samweli akasema, “Nini basi huu mlio wa kondoo masikioni mwangu? Huu mlio wa ng’ombe ninaousikia ni kitu gani?” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Samweli akasema, “Nini basi huu mlio wa kondoo masikioni mwangu? Huu mlio wa ng’ombe ninaousikia ni kitu gani?” BIBLIA KISWAHILI Samweli akasema, Maana yake nini basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? |
Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, nichukuaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.