Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




1 Samueli 13:7 - Swahili Revised Union Version

Hata baadhi ya Waebrania walivuka Yordani, wakaingia nchi ya Gadi na Gileadi; lakini Sauli alikuwa angali huko Gilgali, nao watu wote wakamfuata wakitetemeka.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Wengine walivuka mto Yordani mpaka katika nchi ya Gadi na nchi ya Gileadi. Lakini Shauli alikuwa bado huko Gilgali na watu wote walimfuata wakitetemeka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Wengine walivuka mto Yordani mpaka katika nchi ya Gadi na nchi ya Gileadi. Lakini Shauli alikuwa bado huko Gilgali na watu wote walimfuata wakitetemeka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Wengine walivuka mto Yordani mpaka katika nchi ya Gadi na nchi ya Gileadi. Lakini Shauli alikuwa bado huko Gilgali na watu wote walimfuata wakitetemeka.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hata baadhi ya Waebrania wakavuka Yordani hadi nchi ya Gadi na Gileadi. Sauli akabaki huko Gilgali, navyo vikosi vyote vilivyokuwa pamoja naye vilikuwa vikitetemeka kwa hofu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hata baadhi ya Waebrania wakavuka Yordani mpaka nchi ya Gadi na Gileadi. Sauli akabaki huko Gilgali, navyo vikosi vyote vilivyokuwa pamoja naye vilikuwa vikitetemeka kwa hofu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Hata baadhi ya Waebrania walivuka Yordani, wakaingia nchi ya Gadi na Gileadi; lakini Sauli alikuwa angali huko Gilgali, nao watu wote wakamfuata wakitetemeka.

Tazama sura
Tafsiri zingine



1 Samueli 13:7
15 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.


Tena maofisa na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake.


BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huku na huko katika falme zote za duniani.


Na nchi hiyo tuliitwaa ikawa milki yetu, wakati huo; kutoka Aroeri iliyo kwenye bonde la Arnoni, na nusu ya nchi ya milima ya Gileadi, na miji iliyokuwamo, niliwapa Wareubeni na Wagadi;


na Gileadi na mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na mlima wa Hermoni wote, na Bashani yote mpaka Saleka;


Pamoja na yeye, Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyowapa;


Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu yeyote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu elfu ishirini na mbili wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi.


Akangoja siku saba, kwa kadiri ya muda uliowekwa na Samweli lakini Samweli hakuja Gilgali; na hao watu wakatawanyika mbali naye.


Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana.


Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng'ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.