Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema BWANA; lakini fungu la tatu litabaki humo.
1 Samueli 13:21 - Swahili Revised Union Version Na walilipa theluthi mbili za shekeli kunoa jembe na miundu, na theluthi moja ya shekeli kunoa mashoka na kuchonga michokoo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli walikuwa wanalipa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa wembe wa plau na sururu. Na bei ya kunoa shoka au kupata mchokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli walikuwa wanalipa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa wembe wa plau na sururu. Na bei ya kunoa shoka au kupata mchokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waisraeli walikuwa wanalipa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa wembe wa plau na sururu. Na bei ya kunoa shoka au kupata mchokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli. Neno: Bibilia Takatifu Bei ilikuwa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa majembe ya plau na majembe ya mkono, na theluthi moja ya shekeli kunoa uma, na shoka, na mchokoo. Neno: Maandiko Matakatifu Bei ilikuwa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa majembe ya plau na majembe ya mkono, na theluthi moja ya shekeli kwa nyuma, mashoka na michokoo. BIBLIA KISWAHILI Na walilipa theluthi mbili za shekeli kunoa jembe na miundu, na theluthi moja ya shekeli kunoa mashoka na kuchonga michokoo. |
Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema BWANA; lakini fungu la tatu litabaki humo.
lakini Waisraeli wote hushuka kwa Wafilisti, ili kunoa kila mtu jembe lake, na mundu wake, na shoka lake, na sululu yake;
Hivyo ikawa, siku ya vita, haukuonekana mkononi mwa mtu yeyote, miongoni mwa watu waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani, upanga wala mkuki; isipokuwa Sauli mwenyewe na mwanawe Yonathani walikuwa navyo.