Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 13:8 - Swahili Revised Union Version

8 Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema BWANA; lakini fungu la tatu litabaki humo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Theluthi mbili za watu katika nchi zitaangamizwa; ni theluthi moja tu itakayosalimika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Theluthi mbili za watu katika nchi zitaangamizwa; ni theluthi moja tu itakayosalimika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Theluthi mbili za watu katika nchi zitaangamizwa; ni theluthi moja tu itakayosalimika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 katika nchi yote,” asema Mwenyezi Mungu, “theluthi mbili watapigwa na kuangamia; hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 katika nchi yote,” asema bwana, “theluthi mbili watapigwa na kuangamia; hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema BWANA; lakini fungu la tatu litabaki humo.

Tazama sura Nakili




Zekaria 13:8
34 Marejeleo ya Msalaba  

Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.


Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.


Maana mimi ni pamoja nawe, asema BWANA, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.


Nami nitawasafisha kwa kuwatoa waasi, na hao walionikosa; nitawatoa katika nchi wanayokaa ugenini, lakini hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.


Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.


Wenye dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, Mabaya hayatatupata nyuma wala mbele.


Lakini nitabakiza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la BWANA.


Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.


Basi yule mfalme akaghadhibika; akatuma majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.


Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.


Na mji ule mkuu ukagawanyika katika mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo