1 Samueli 12:6 - Swahili Revised Union Version Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, yeye ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Samueli akawaambia, “Mwenyezi-Mungu ndiye aliyemteua Mose na Aroni na kuwatoa babu zenu nchini Misri. Biblia Habari Njema - BHND Samueli akawaambia, “Mwenyezi-Mungu ndiye aliyemteua Mose na Aroni na kuwatoa babu zenu nchini Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Samueli akawaambia, “Mwenyezi-Mungu ndiye aliyemteua Mose na Aroni na kuwatoa babu zenu nchini Misri. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Samweli akawaambia watu, “Mwenyezi Mungu ndiye alimchagua Musa na Haruni, na kuwaleta baba zenu akiwapandisha kutoka Misri. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Samweli akawaambia watu, “bwana ndiye alimchagua Musa na Haruni, na kuwaleta baba zenu akiwapandisha kutoka Misri. BIBLIA KISWAHILI Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, yeye ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri. |
Musa na Haruni walikuwa makuhani wake, Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake, Walimlilia BWANA naye akawaitikia;
Hawa ni Haruni yeye yule, na Musa yeye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao.
Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa yeye yule, na Haruni yeye yule.
Kwa maana nilikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami niliwatuma Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako.