Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
1 Samueli 12:16 - Swahili Revised Union Version Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo basi, tulieni na kulitazama jambo hilo kubwa ambalo Mwenyezi-Mungu atatenda mbele yenu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo basi, tulieni na kulitazama jambo hilo kubwa ambalo Mwenyezi-Mungu atatenda mbele yenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo basi, tulieni na kulitazama jambo hilo kubwa ambalo Mwenyezi-Mungu atatenda mbele yenu. Neno: Bibilia Takatifu “Sasa basi, simameni kimya mkaone jambo hili kubwa ambalo Mwenyezi Mungu anaenda kulifanya mbele ya macho yenu! Neno: Maandiko Matakatifu “Sasa basi, simameni kimya mkaone jambo hili kubwa ambalo bwana anakwenda kulifanya mbele ya macho yenu! BIBLIA KISWAHILI Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. |
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.
Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu.
Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia BWANA usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema.