Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea dada yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.
1 Samueli 1:6 - Swahili Revised Union Version Ila mwenzake humchokoza sana, ili kumwuudhi, kwa sababu BWANA alikuwa amemfunga tumbo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Penina, mchokozi wa Hana, daima alikuwa akimkasirisha vikali na kumuudhi Hana kwa kuwa Mwenyezi-Mungu hakumjalia watoto. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Penina, mchokozi wa Hana, daima alikuwa akimkasirisha vikali na kumuudhi Hana kwa kuwa Mwenyezi-Mungu hakumjalia watoto. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Penina, mchokozi wa Hana, daima alikuwa akimkasirisha vikali na kumuudhi Hana kwa kuwa Mwenyezi-Mungu hakumjalia watoto. Neno: Bibilia Takatifu Kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa amemfunga tumbo, mke mwenzake alikuwa anamchokoza ili kumuudhi. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa sababu bwana alikuwa amemfunga tumbo, mke mwenzake alikuwa anamchokoza ili kumuudhi. BIBLIA KISWAHILI Ila mwenzake humchokoza sana, ili kumwuudhi, kwa sababu BWANA alikuwa amemfunga tumbo. |
Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea dada yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.
Kwake huyo atakaye kuzima roho inapasa atendewe mema na rafiki; Hata kwake huyo aachaye kumcha Mwenyezi.
Wala usitwae mwanamke pamoja na dada yake, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, dada yake akiwa hai.
Kisha akamwambia baba yake, Basi na nifanyiwe neno hili; niache peke yangu muda wa miezi miwili, ili nipate kwenda milimani, na kuombolea ubikira wangu, mimi na wenzangu.
Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa BWANA, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula.
Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;