Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
1 Petro 1:16 - Swahili Revised Union Version kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maandiko yasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi alivyo mtakatifu.” Biblia Habari Njema - BHND Maandiko yasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi alivyo mtakatifu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maandiko yasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi alivyo mtakatifu.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana imeandikwa: “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana imeandikwa: “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” BIBLIA KISWAHILI kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. |
Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya nchi.
Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.
Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu.