Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


109 Mistari ya Biblia kuhusu Kukataliwa

109 Mistari ya Biblia kuhusu Kukataliwa

Rafiki yangu, najua ya kwamba sote tunaweza kukumbana na wakati mgumu wa kukatishwa tamaa na kuhisi kukataliwa, hasa baada ya uhusiano wa kimapenzi kuvunjika. Inauma sana, na ni sawa kuhisi hivyo.

Lakini unajua, tuna jambo la muhimu sana linalotupa faraja na mwangaza katika nyakati kama hizi: Neno la Mungu. Biblia inatukumbusha kwamba thamani yetu haitegemei maoni ya mtu mmoja. Mungu anatupenda sisi sote bila kujali.

Kukataliwa kunaweza kutufanya tujisikie wapweke na duni, lakini tunaweza kuchagua kutokubali hisia hizo zitawale. Badala yake, tunaweza kumgeukia Mungu kwa ajili ya nguvu. Yeye ndiye kimbilio letu.

Hebu tumwombe Mungu atupe uhuru kutoka katika maumivu haya. Tukumbuke kwamba upendo wake hauna mwisho na unatukubali sisi jinsi tulivyo. Hata tukihisi tumeachwa na wengine, Mungu yuko nasi sikuzote.


Zaburi 94:14

Mwenyezi-Mungu hatawaacha watu wake; hatawatupa hao walio mali yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 27:10

Hata kama wazazi wangu wakinitupa, Mwenyezi-Mungu atanipokea kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 15:18

“Kama ulimwengu ukiwachukia nyinyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla ya kuwachukia nyinyi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Maombolezo 3:31

Mwenyezi-Mungu hatatutupa milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 1:11

Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 12:9

Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 53:3

Alidharauliwa na kukataliwa na watu, alikuwa mtu wa uchungu na huzuni. Alikuwa kama mtu kinyaa kwa watu; alidharauliwa na tukamwona si kitu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 34:17-18

Waadilifu wakimlilia Mwenyezi-Mungu yeye huwasikia, na kuwaokoa katika taabu zao zote. Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo; huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:23-24

Mwenyezi-Mungu huziongoza nyayo za mtu, humlinda yule ampendezaye. Ajapoanguka, haanguki akabaki chini, kwa sababu Mwenyezi-Mungu humtegemeza.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Samueli 16:7

Lakini Mwenyezi-Mungu alimwambia, “Usiangalie sura yake na urefu wa kimo chake. Mimi nimemkataa kwani siangalii mambo kama wanavyoyaangalia binadamu wenye kufa. Binadamu huangalia uzuri wa nje, lakini mimi naangalia moyoni.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 51:17

tambiko yangu kwako ee Mungu, ni moyo mnyofu; wewe, ee Mungu, hukatai moyo mnyofu na mtiifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 10:16

Halafu akasema, “Anayewasikiliza nyinyi, ananisikiliza mimi; na anayekataa kuwapokea nyinyi, anakataa kunipokea mimi. Na yeyote anayekataa kunipokea, anakataa kumpokea yule aliyenituma.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 17:25

Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 56:3-4

Ee Mungu Mkuu, hofu inaponishika, mimi nakutumainia wewe. Namtumainia Mungu na kusifu neno lake; namtumainia Mungu, wala siogopi. Binadamu dhaifu atanifanya nini?

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 118:2

Watu wa Israeli na waseme: “Fadhili zake zadumu milele.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 4:4

Kila kitu alichoumba Mungu ni chema, wala hakuna kinachohitaji kukataliwa, bali vyote vipokelewe kwa sala ya shukrani,

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 54:6

“Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema:

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 2:4

Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 139:13-14

Wewe umeniumba, mwili wangu wote; ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu. Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:11-12

Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu, wala usiudhike kwa maonyo yake; maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye, kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 118:22

Jiwe walilokataa waashi, limekuwa jiwe kuu la msingi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 49:15-16

Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Je, mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya, asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake? Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe, mimi kamwe sitakusahau. Nimekuchora katika viganja vyangu; kuta zako naziona daima mbele yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 54:4-5

Usiogope maana hutaaibishwa tena; usifadhaike maana hutadharauliwa tena. Utaisahau aibu ya ujana wako, wala hutaikumbuka tena fedheha ya ujane wako. Muumba wako atakuwa mume wako; Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; yeye aitwa ‘Mungu wa ulimwengu wote’.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 55:8-9

Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mawazo yangu si kama mawazo yenu, wala njia zangu si kama njia zenu. Kama vile mbingu zilivyo mbali na dunia, ndivyo njia zangu zilivyo mbali na zenu, na mawazo yangu mbali na mawazo yenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 61:1-3

Bwana Mwenyezi-Mungu amenijaza roho yake, maana Mwenyezi-Mungu ameniweka wakfu, akanituma niwaletee wanaokandamizwa habari njema, niwatibu waliovunjika moyo, niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa. Nitafurahi sana kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu. Maana amenivika vazi la wokovu, amenivalisha vazi la uadilifu, kama bwana arusi ajipambavyo kwa shada la maua, kama bibi arusi ajipambavyo kwa johari zake. Hivyo, kama vile ardhi ioteshavyo mimea, na shamba lichipushavyo mbegu zilizopandwa humo, Mwenyezi-Mungu atasababisha uadilifu na sifa kuchomoza mbele ya mataifa yote. Amenituma niutangaze mwaka wake wa neema, na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi; niwafariji wote wanaoomboleza; niwape wale wanaoomboleza katika Siyoni taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya moyo mzito. Nao wataitwa mialoni madhubuti, aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 66:5

Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu, enyi msikiao neno lake mkatetemeka: “Ndugu zenu ambao wanawachukia, na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu, wamesema kwa dharau ‘Mungu na aoneshe utukufu wake, nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’ Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 1:5

“Kabla hujachukuliwa mimba, mimi nilikujua, kabla hujazaliwa, mimi nilikuweka wakfu; nilikuteua uwe nabii kwa mataifa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 29:11

Maana, mimi Mwenyezi-Mungu ninajua mambo niliyowapangia. Nimewapangieni mema na si mabaya, ili mpate kuwa na tumaini la baadaye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 31:3

mimi Mwenyezi-Mungu nilimtokea kwa mbali. Nami nimekupenda kwa mapendo ya daima, kwa hiyo nimeendelea kuwa mwaminifu kwako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Maombolezo 3:22-23

Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno.

Sura   |  Matoleo Nakili
Maombolezo 3:31-33

Mwenyezi-Mungu hatatutupa milele. Ingawa atufanya tuhuzunike, atakuwa na huruma tena kadiri ya wingi wa fadhili zake. Yeye hapendelei kuwatesa wala kuwahuzunisha wanadamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hosea 6:1

“ ‘Twendeni, tukamrudie Mwenyezi-Mungu! Yeye mwenyewe ameturarua, lakini yeye mwenyewe atatuponya. Yeye mwenyewe ametujeruhi, lakini yeye mwenyewe atatibu majeraha yetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mika 7:8

Usifurahie maafa yangu ewe adui yangu! Nikianguka, nitainuka tena; Nikiwa gizani, Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:10-12

Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao. “Heri yenu nyinyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 10:14

Kama mtu yeyote atakataa kuwakaribisheni au kuwasikilizeni, basi mtokapo katika nyumba hiyo au mji huo, yakunguteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 11:28-30

Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu. wamwulize: “Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?” Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 21:42

Hapo Yesu akawaambia, “Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko Matakatifu? ‘Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi. Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu!’

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 27:46

Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, “Eli, Eli, lema sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 8:31

Yesu alianza kuwafundisha wanafunzi wake kwamba ni lazima Mwana wa Mtu apatwe na mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Kwamba atauawa, na baada ya siku tatu atafufuka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 6:22-23

“Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu. Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 9:5

Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kunguteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 3:16-17

Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uhai wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 6:37

Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami kamwe sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 7:7

Ulimwengu hauwezi kuwachukia nyinyi, lakini mimi wanichukia kwa sababu mimi nashuhudia juu yake kwamba matendo yake ni maovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 15:18-19

“Kama ulimwengu ukiwachukia nyinyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla ya kuwachukia nyinyi. Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda nyinyi kama watu wake. Lakini kwa vile nyinyi si wa ulimwengu, ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 16:33

Nimewaambieni mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 4:11

Huyu ndiye ambaye Maandiko Matakatifu yanasema: ‘Jiwe mlilokataa nyinyi waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 7:35

“Huyu Mose ndiye yule watu wa Israeli waliyemkataa waliposema: ‘Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wetu?’ Kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto, Mungu alimtuma Mose huyo awe kiongozi na mkombozi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 9:15

Lakini Bwana akamwambia, “Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa watu wa Israeli.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 5:3-5

Naam, si hayo tu, bali tunafurahi pia katika taabu tukijua kwamba taabu huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti, na uthabiti huleta tumaini. Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha mimina mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:1

Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu kwa wale ambao katika maisha yao wameungana na Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:31

Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga?

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:38-39

Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 9:33

kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Tazama, nitaweka huko Siyoni jiwe likwazalo, mwamba utakaowafanya watu waanguke. Lakini atakayemwamini hataaibishwa!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:2

Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 1:28

Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikira za dunia ni mambo yaliyo duni na yanayodharauliwa, mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo ayafutilie mbali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo ya maana.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 15:10

Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 1:3-4

Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote. Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 4:8-9

Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka, lakini hatukati tamaa; twateseka, lakini hatuachwi bila msaada; na ingawa tumeangushwa chini, hatukuangamizwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 5:17

Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 1:10

Sasa nataka kibali cha nani: Cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 2:20

na sasa naishi, lakini si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha haya ninayoishi sasa naishi kwa imani, imani katika Mwana wa Mungu aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 1:4-5

Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituteua tuwe wake katika kuungana na Kristo ili tuwe watakatifu na bila hitilafu mbele yake. Kwa sababu ya upendo wake, Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 1:6

Basi, tumsifu Mungu kwa sababu ya neema yake tukufu ambayo ametujalia katika Mwanae mpenzi!

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 2:10

Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 2:19

Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 3:12

Basi, kwa kuungana na Kristo na kwa imani kwake, sisi tunathubutu kumwendea Mungu kwa matumaini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:13

Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 1:13-14

Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi. Kwake yeye tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:3

Maana nyinyi mmekufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:23-24

Mungu mwenyewe anayetupatia amani awatakase nyinyi kabisa kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu – roho, mioyo na miili yenu – mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye anayewaita nyinyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wathesalonike 2:16-17

Tunamwomba Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu ambaye alitupenda na kwa neema yake akatujalia faraja ya milele na tumaini jema, aifariji mioyo yenu na kuwaimarisheni ili muweze daima kutenda na kusema yaliyo mema.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 1:7

Kwa maana Roho tuliyepewa na Mungu si wa kutufanya tuwe waoga; sivyo, ila ni Roho wa kutujalia upendo na nidhamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 4:16-17

Wakati nilipojitetea kwa mara ya kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu; wote waliniacha. Mungu asiwahesabie kosa hilo! Lakini Bwana alikaa pamoja nami, akanipa nguvu, hata nikaweza kuutangaza ujumbe wote, watu wa mataifa wausikie; tena nikaokolewa katika hukumu ya kifo kama kinywani mwa simba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 4:15-16

Huyu Kuhani Mkuu wetu anaelewa kabisa unyonge wetu; yeye mwenyewe alijaribiwa kama sisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi. Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu mwenye neema, tupokee huruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:35-36

Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatia tuzo kubwa. Mnahitaji kuwa na uvumilivu ili muweze kutimiza matakwa ya Mungu na kupokea kile alichoahidi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:5-6

Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.” Ndiyo maana tunathubutu kusema: “Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 1:2-4

Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki. Kwa hiyo, tupilieni mbali mwenendo mchafu na tabia zote mbovu; jiwekeni chini ya Mungu na kupokea lile neno lililopandwa mioyoni mwenu, ambalo laweza kuziokoa nafsi zenu. Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo. Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo. Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo. Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya. Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe. Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu. kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu. Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 4:7-8

Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye atawakimbieni. Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki!

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 2:4-5

Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa. Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea tambiko za kiroho zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 3:14

Lakini, hata kama itawapasa kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, basi, mna heri. Msimwogope mtu yeyote, wala msikubali kutiwa katika wasiwasi.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 5:7

Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 5:10

Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 3:1

Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 4:4

Lakini nyinyi, watoto, ni wake Mungu na mmekwisha washinda hao manabii wa uongo; maana Roho aliye ndani yenu ana nguvu kuliko roho aliye ndani ya hao walio wa ulimwengu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 4:18-19

Palipo na upendo hapana woga; naam, upendo kamili hufukuza woga wote. Basi, mtu mwenye woga hajakamilika bado katika upendo, kwani woga huhusikana na adhabu. Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 5:4

maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: Kwa imani yetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 66:20

Asifiwe Mungu, maana hakuikataa sala yangu, wala kuondoa fadhili zake kwangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 147:3

Anawaponya waliovunjika moyo; na kuwatibu majeraha yao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 26:3

Ee Mungu, wawaweka katika amani walio thabiti, wawaweka katika amani kwa kuwa wanakutegemea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 43:1-2

Mwenyezi-Mungu aliyewaumba enyi watu wa Yakobo, yeye aliyewafanya enyi watu wa Israeli, asema: “Msiogope, maana mimi nimewakomboa; nimewaita kwa jina nanyi ni wangu. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nyinyi Waisraeli ni mashahidi wangu; niliwachagua muwe watumishi wangu, mpate kunijua na kuniamini, kwamba ndimi peke yangu Mungu. Kabla yangu hajapata kuwapo mungu mwingine, wala hatakuwapo mungu mwingine. “Mimi peke yangu ndimi Mwenyezi-Mungu, hakuna mkombozi mwingine ila mimi. Nilitangaza yale ambayo yangetukia, kisha nikaja na kuwakomboa. Hakuna mungu mwingine aliyewahi kufanya hivyo, nanyi ni mashahidi wangu. Mimi ni Mungu na nitakuwa Mungu daima. Hakuna awezaye kuiepa nguvu yangu; hakuna awezaye kupinga ninayofanya.” Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi: “Kwa ajili yenu nitatuma jeshi Babuloni. Nitayavunjilia mbali malango ya mji wake, na kelele za hao Wakaldayo zitageuka maombolezo. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wenu; Mimi ndimi Muumba wa Israeli, Mfalme wenu.” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati mmoja nilifanya barabara baharini nikaweka njia kati ya mawimbi makubwa. Nililipiga jeshi lenye nguvu, jeshi la magari na farasi wa vita, askari na mashujaa wa vita. Niliwaangusha chini wasiweze kuinuka tena, niliwakomesha na kuwazima kama utambi wa taa. Sasa nasema: ‘Msiyanganganie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani. Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya. Kinafanyika sasa hivi, nanyi mtaweza kukiona. Nitafanya njia nyikani, na kububujisha mito jangwani. Mkipita katika mafuriko, mimi nitakuwa pamoja nanyi; mkipita katika mito, haitawashinda nguvu. Mkitembea katika moto, hamtaunguzwa; mwali wa moto hautawaunguza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 55:22

Mwachie Mwenyezi-Mungu mzigo wako, naye atakutegemeza; kamwe hamwachi mwadilifu ashindwe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:5

Mkabidhi Mwenyezi-Mungu maisha yako; mtumainie yeye naye atafanya kitu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 138:8

Ee Mwenyezi-Mungu, utatimiza yote uliyoniahidi. Fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, zadumu milele. Usisahau kazi ya mkono wako mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 62:8

Enyi watu, mtumainieni Mungu daima; mfungulieni Bwana yaliyo moyoni mwenu. Mungu ndiye kimbilio la usalama wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 40:31

Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 46:1-2

Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu. Asema: “Nyamazeni na kujua kuwa mimi ni Mungu! Mimi natukuka katika mataifa yote; mimi natukuzwa ulimwenguni kote!” Mwenyezi-Mungu wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu. Kwa hiyo hatutaogopa chochote, dunia ijapoyeyuka na milima kutikisika kutoka baharini;

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 6:33

Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:1

Yesu aliwaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:19

Basi, Mungu wangu, kwa utajiri wake mkuu kwa njia ya Kristo, atawapeni mahitaji yenu yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 17:7-8

“Abarikiwe mtu anayemtegemea Mwenyezi-Mungu, mtu ambaye Mwenyezi-Mungu ndiye tegemeo lake. Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya maji, upenyezao mizizi yake karibu na chemchemi. Hauogopi wakati wa joto ufikapo, majani yake hubaki mabichi. Hauhangaiki katika mwaka wa ukame, na hautaacha kuzaa matunda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 31:24

Muwe hodari na kupiga moyo konde, enyi nyote mnaomtumainia Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 55:6-7

Mtafuteni Mwenyezi-Mungu wakati bado anapatikana, mwombeni msaada wakati yupo bado karibu. Waovu na waache njia zao mbaya, watu wabaya waachane na mawazo yao mabaya; wamrudie Mwenyezi-Mungu apate kuwahurumia, wamwendee Mungu wetu maana atawasamehe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:12

Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 4:23

Linda moyo wako kwa uangalifu wote, maana humo zatoka chemchemi za uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 2:9

Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu.

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu mwema wa milele, Bwana Mkuu! Nakusifu kwa sababu wewe ni Mwadilifu, Mtakatifu na unastahili sifa na kuabudiwa kuu. Baba, nifundishe kila siku kukaa katika uwepo wako na kuelewa kwamba wewe ni mfano wangu mkuu, kwamba kukataliwa hakunifafanui, bali kunanilenga zaidi katika kusudi langu. Nifunze kuwa kama wewe, ili jambo muhimu zaidi kwangu liwe kutimiza mapenzi ya Baba, wala si kupendwa na wanadamu, kwani ulikuja kwa walio wako nao hawakukukaribisha. Nisaidie kusimama imara dhidi ya kukataliwa, nisijiache nidharauliwe wala kuogopeshwa na mashambulizi ya adui, kwani hukunipa roho ya woga, bali ya upendo, nguvu na nidhamu. Asante Baba, kwa sababu umenipa utambulisho wa mtoto wa Mungu na umenilinda na Roho wako Mtakatifu ili kushinda hofu na wasiwasi, leo nakuomba ulinde moyo wangu na unipe nguvu na ujasiri ili nisikubali kukataliwa kutoboa moyo wangu. Nifanye nielewe kwamba niliumbwa kwa kusudi na kwamba dharau ni sehemu yake katika maisha yangu. Leo nakataa mawazo yote ya kushindwa na kukata tamaa, najitangaza huru katika jina la Yesu. Amina!
Tufuate:

Matangazo


Matangazo