Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


65 Mistari ya Biblia kuhusu Lugha

65 Mistari ya Biblia kuhusu Lugha

Rafiki yangu, si ajabu jinsi neno la Mungu limeenea kote duniani, hata limefika kwetu katika lugha yetu wenyewe? Biblia inatuambia jinsi lugha zilivyoanza, na ni jambo la kushangaza kuona jinsi ujumbe wake umefasiriwa katika lugha nyingi sana.

Tuna bahati kubwa sisi Wakristo, kuwa na Biblia katika lugha tunayoielewa vvizuri. Inakuwa kama ngome yetu, hasa wakati wa shida, tunapohisi kama hakuna anayetuelewa. Katika nyakati hizo ngumu, tunakumbuka kwamba Mungu anatufahamu, anasikia kilio chetu katika lugha yetu. Tukijikumbatia katika neno lake, tunapata faraja, tunapata moyo, na tunapata mwongozo. Hata matatizo yanayotukabili, tunaweza kupata suluhisho kupitia Biblia.

Kitabu hiki kitakatifu ni kama mwongozo wa maisha yetu. Kinatuonyesha njia inayofaa, kinatuonya juu ya mambo ya kuepukana nayo. Kwa kweli, tumebarikiwa sana. Mungu, katika rehema zake zisizo na mwisho, ametupa sisi wanadamu uwezo wa kuwasiliana, bila kujali wapi duniani tunapopatikana.


Waroma 14:11

Maana Maandiko yanasema: “Kama niishivyo, asema Bwana, kila mtu atanipigia magoti, na kila mmoja atakiri kwamba mimi ni Mungu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 11:1-9

Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale. Wafuatao ni wazawa wa Shemu. Miaka miwili baada ya ile gharika, Shemu akiwa na umri wa miaka 100, alimzaa Arfaksadi. Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Arfaksadi alipokuwa na umri wa miaka 35, alimzaa Shela. Baada ya kumzaa Shela, Arfaksadi aliishi miaka 403 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Shela alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Eberi. Baada ya kumzaa Eberi, Shela aliishi miaka 403 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Eberi alipokuwa na umri wa miaka 34, alimzaa Pelegi. Baada ya kumzaa Pelegi, Eberi aliishi miaka 430 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Pelegi alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Reu. Baada ya kumzaa Reu, Pelegi aliishi miaka 209 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Basi, ikawa watu waliposafirisafiri kutoka mashariki, walifika katika nchi tambarare huko Shinari, wakakaa. Reu alipokuwa na umri wa miaka 32, alimzaa Serugi. Baada ya kumzaa Serugi, Reu aliishi miaka 207 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Serugi alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Nahori. Baada ya kumzaa Nahori, Serugi aliishi miaka 200 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Nahori alipokuwa na umri wa miaka 29, alimzaa Tera. Baada ya kumzaa Tera, Nahori aliishi miaka 119, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Tera alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Abramu na Nahori na Harani. Wafuatao ni wazawa wa Tera, baba yao Abramu, Nahori na Harani. Harani alikuwa baba yake Loti. Huyo Harani alifariki wakati Tera baba yake alikuwa anaishi huko Uri alikokuwa amezaliwa. Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai. Mke wa Nahori aliitwa Milka, binti Harani ambaye pia alikuwa baba yake Iska. Kisha wakaambiana, “Haya! Na tufyatue matofali, tuyachome moto vizuri.” Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Sarai hakuwa na mtoto kwa sababu alikuwa tasa. Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mjukuu wake aliyekuwa mwanawe Harani, na Sarai mkewe Abramu, wakaondoka wote pamoja toka Uri, mji wa Wakaldayo, wakaenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakakaa. Tera alifariki huko Harani akiwa na umri wa miaka 205. Wakasema, “Na tujijengee mji na mnara ambao kilele chake kitafika mbinguni ili tujipatie jina, tusije tukatawanyika duniani kote.” Ndipo Mwenyezi-Mungu akashuka chini kuuona mji huo na mnara walioujenga binadamu. Mwenyezi-Mungu akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na wote wana lugha moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayoyafanya. Lolote wanalokusudia kulifanya watafanikiwa. Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” Hivyo, Mwenyezi-Mungu akawatawanya mahali pote duniani, nao wakaacha kuujenga ule mji. Mji huo ukaitwa Babeli, kwa sababu huko ndiko Mwenyezi-Mungu alikoivuruga lugha ya dunia yote, na kutoka huko akawatawanya watu kila mahali duniani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 17:7

Maneno mazuri si kawaida kinywani mwa mpumbavu, sembuse maneno ya uongo kinywani mwa kiongozi!

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 11:6-7

Mwenyezi-Mungu akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na wote wana lugha moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayoyafanya. Lolote wanalokusudia kulifanya watafanikiwa. Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 81:5

Aliwapa watu wa Israeli agizo hilo, alipoishambulia nchi ya Misri. Nasikia sauti nisiyoitambua ikisema:

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 19:3-4

Hamna msemo au maneno yanayotumika; wala hakuna sauti inayosikika; hata hivyo, sauti yao yaenea duniani kote, na maneno yao yafika kingo za ulimwengu. Mungu ameliwekea jua makao yake angani;

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 28:49

“Mwenyezi-Mungu ataleta kutoka mbali taifa moja liwavamie kasi kama tai, taifa ambalo lugha yake hamuielewi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 28:11

Haya basi! Mwenyezi-Mungu ataongea na watu hawa kwa njia ya watu wa lugha tofauti wanaoongea lugha ngeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 33:19

Hamtawaona tena watu wale wenye kiburi, wanaozungumza lugha isiyoeleweka.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 14:39-40

Hivyo basi, ndugu zangu, mnapaswa kuwa na hamu ya kutangaza ujumbe wa Mungu; lakini msimkataze mtu kusema kwa lugha ngeni. Mwenye kunena lugha ngeni anajijenga mwenyewe. Lakini mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, analijenga kanisa. Lakini yote yafanyike kwa heshima na kwa utaratibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:6

Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kadiri ya neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Danieli 3:4-5

Mpiga mbiu akatangaza kwa sauti kubwa, “Enyi watu wa makabila yote, mataifa yote na lugha zote, mnaamriwa kwamba mkisikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, lazima mwiname chini na kuiabudu sanamu ya dhahabu aliyosimamisha mfalme Nebukadneza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 3:1-12

Ndugu zangu, wengi wenu msiwe waalimu. Kama mjuavyo, sisi waalimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine. Maneno ya kubariki na ya kulaani hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo. Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu pamoja? Ndugu zangu, je, mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Danieli 5:25-28

“Maandishi yenyewe ni: ‘MENE, MENE, TEKELI, PARSINI.’ Na hii ndiyo maana yake: MENE maana yake, Mungu amehesabu siku za ufalme wako na kuukomesha. TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. PERESI maana yake, ufalme wako umegawanywa kati ya Wamedi na Wapersi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 28:19

Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 16:17

Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 2:4-6

Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowawezesha. Kwa maneno mengine mengi, Petro alisisitiza na kuwahimiza watu akisema, “Jiokoeni katika kizazi hiki kiovu.” Wengi waliyakubali maneno yake, wakabatizwa. Watu wapatao 3,000 wakaongezeka katika kile kikundi siku hiyo. Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali. Miujiza na maajabu mengi yalifanyika kwa njia ya mitume hata kila mtu akajawa na hofu. Waumini wote waliendelea kuwa kitu kimoja na mali zao waligawiana. Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja. Waliendelea kukutana pamoja kila siku hekaluni. Lakini wakati wa kumega mkate, walikutana katika nyumba zao na wakakishiriki chakula hicho kwa furaha na moyo mkunjufu. Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa. Na huko Yerusalemu walikuwako Wayahudi, watu wamchao Mungu, waliotoka katika kila nchi duniani. Waliposikia sauti hiyo, kundi kubwa la watu lilikusanyika. Wote walishtuka sana kwani kila mmoja wao aliwasikia hao waumini wakisema kwa lugha yake mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 3:28

Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:11

Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu, na yumo katika yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 10:46

maana waliwasikia wakiongea kwa lugha mbalimbali wakimtukuza Mungu. Hapo Petro akasema,

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 4:29

Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 19:6

Basi, Paulo akawawekea mikono, na Roho Mtakatifu akawashukia, wakaanza kusema lugha ngeni na kutangaza ujumbe wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 12:10

humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzifafanua.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 145:17

Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu katika njia zake zote; ni mwema katika matendo yake yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 66:16

Enyi mnaomcha Mungu, njoni nyote mkasikilize, nami nitawasimulieni aliyonitendea.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 12:28

Mungu ameweka katika kanisa: Kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 13:1

Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 18:21

Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua; wanaopenda kuutumia watakula matunda yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 14:2

Mwenye kunena lugha ngeni hasemi na watu bali anasema na Mungu. Yeye hunena kwa nguvu ya Roho mambo yaliyofichika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:11

na kila mtu akiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 15:6

ili nyinyi nyote, kwa nia moja na sauti moja, mumtukuze Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 14:5

Basi, ningependa nyinyi nyote mseme kwa lugha ngeni lakini ningependelea hasa muwe na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, maana mtu mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni wa maana zaidi kuliko yule mwenye kusema lugha ngeni, isipokuwa tu kama yupo hapo mtu awezaye kuyafafanua hayo mambo asemayo, ili kanisa lipate kujengwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 14:10-11

Zipo lugha mbalimbali ulimwenguni, na hakuna hata mojawapo isiyo na maana. Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayo mtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye pia ni mgeni kwangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 4:11

Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 14:18-19

Namshukuru Mungu kwamba mimi nasema kwa lugha ngeni kuliko nyinyi nyote. Lakini katika mikutano ya waumini napendelea zaidi kusema maneno matano yenye kueleweka ili niwafundishe wengine, kuliko kusema maneno elfu ya lugha ngeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 2:38-39

Petro akajibu, “Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile ahadi ya Roho Mtakatifu. Maana, ahadi ile ilikuwa kwa ajili yenu, kwa ajili ya watoto wenu, kwa ajili ya wote wanaokaa mbali na kwa ajili ya kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita kwake.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 12:34-37

Enyi kizazi cha nyoka! Mnawezaje kusema mambo mema hali nyinyi ni waovu? Maana mtu husema kutokana na yale yaliyojaa moyoni. Mtu mwema hutoa mambo mema katika hazina yake njema; na mtu mbaya hutoa mambo mabaya katika hazina yake mbaya. “Basi, nawaambieni, siku ya hukumu watu watapaswa kujibu juu ya kila neno lisilofaa wanalosema. Maana kwa maneno yako utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno yako utahukumiwa kuwa na hatia.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 14:21-22

Imeandikwa katika sheria: “Bwana asema hivi: ‘Kwa njia ya wenye kunena lugha ngeni, na kwa midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, hata hivyo, hawatanisikiliza.’” Hivyo basi, kipaji cha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwa ajili ya watu wenye imani, bali kwa ajili ya wale wasioamini; lakini kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni kwa ajili ya wale wanaoamini na si kwa ajili ya wasioamini.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 14:26-28

Ndugu, tuseme nini, basi? Mnapokutana pamoja, mmoja aimbe wimbo, mwingine atoe mafundisho, mwingine awe na ufunuo kutoka kwa Mungu, mwingine atumie kipaji cha kusema kwa lugha ngeni na mwingine afafanue yanayosemwa. Yote yawe kwa ajili ya kulijenga kanisa. Wakiwapo watu wenye vipaji vya kusema kwa lugha ngeni, waseme wawili au watatu, si zaidi, tena mmojammoja; na aweko mtu wa kufafanua yanayosemwa. Lakini kama hakuna awezaye kufafanua, basi, mwenye kusema lugha ngeni anyamaze mkutanoni, aseme na nafsi yake mwenyewe na Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 7:9

Kisha, nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: Watu wa kila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo, wamevaa mavazi meupe na kushika matawi ya mitende mikononi mwao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:30

Mtu mwadilifu husema maneno ya hekima, kwa ulimi wake hunena yaliyo ya haki.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 10:11

Kisha, nikaambiwa, “Inakubidi tena kutoa unabii kuhusu watu wengi, mataifa, watu wa lugha nyingi na wafalme!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 140:3

Ndimi zao hatari kama za nyoka; midomoni mwao mna maneno ya sumu kama ya joka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 14:6

Kisha, nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote na watu wa lugha zote na rangi zote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 116:10

Nilikuwa na imani hata niliposema: “Mimi nimetaabika mno.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 109:2

Watu waovu na wadanganyifu wanishambulia, wanasema uongo dhidi yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 21:23

Achungaye mdomo wake na ulimi wake, hujiepusha na matatizo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 4:6

Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 8:26-35

Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita jangwani). Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati huohuo kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea nyumbani. Huyo mtu alikuwa mkurugenzi maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo alikuwa anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa. Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya. Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo.” Wakati huohuo, Saulo alijaribu kuliangamiza kanisa. Alikwenda katika kila nyumba, akawatoa nje waumini, wanaume kwa wanawake, akawatia gerezani. Filipo akakimbilia karibu na gari, akamsikia huyo mtu akisoma katika kitabu cha nabii Isaya. Hapo Filipo akamwuliza, “Je, unaelewa hayo unayosoma?” Huyo mtu akamjibu, “Ninawezaje kuelewa bila mtu kuniongoza?” Hapo akamwalika Filipo apande juu, aketi pamoja naye. Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwanakondoo anapokatwa manyoya, yeye hakutoa sauti hata kidogo. Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani.” Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabii anasema juu ya nini? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?” Basi, Filipo akianzia na sehemu hiyo ya Maandiko Matakatifu, akamweleza Habari Njema juu ya Yesu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 24:44-48

Halafu akawaambia, “Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: Kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi.” Kisha, akaziangazia akili zao ili wapate kuelewa Maandiko Matakatifu. Akawaambia, “Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu, na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia Yerusalemu, yahubiriwe kwamba watu wanapaswa kutubu na kusamehewa dhambi. Nyinyi ni mashahidi wa mambo hayo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 28:19-20

Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Ghafla kukatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 11:1

Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 11:7

Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 11:9

Mji huo ukaitwa Babeli, kwa sababu huko ndiko Mwenyezi-Mungu alikoivuruga lugha ya dunia yote, na kutoka huko akawatawanya watu kila mahali duniani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 2:8

Imekuwaje, basi, kwamba kila mmoja wetu anawasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe?

Sura   |  Matoleo Nakili
Danieli 1:4

Mfalme alitaka vijana wasio na kasoro, wazuri kwa umbo, wenye uzoefu wa kila hekima, wenye akili na maarifa na wanaofaa kutoa huduma katika ikulu. Alitaka pia vijana hao wafundishwe kusoma na kuandika lugha ya Wakaldayo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 50:4

Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha, niwatie moyo wale waliochoka. Kila asubuhi hunipa hamu ya kusikiliza anayotaka kunifunza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Nehemia 13:24

na nusu ya watoto wao walizungumza Kiashdodi au lugha nyingine na hawakuweza kuzungumza lugha ya Yuda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waamuzi 12:6

walimwambia: “Haya tamka neno ‘Shibolethi’” lakini yeye hutamka “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kulitamka sawasawa. Hapo, walimkamata, wakamuua huko kwenye vivuko vya mto Yordani. Watu 42,000 wa Efraimu walipoteza maisha yao wakati huo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 10:31

Hao ndio wazawa wa Shemu, kadiri ya makabila yao, lugha zao, nchi zao na mataifa yao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezra 4:7

Tena wakati wa utawala wa Artashasta, mfalme wa Persia, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli na rafiki zao, walimwandikia barua mfalme Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa herufi za Kiaramu na kutafsiriwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wafalme 18:26

Basi, Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia huyo jemadari mkuu, “Tafadhali, sema nasi kwa lugha ya Kiaramu, maana tunaielewa; usiseme nasi kwa lugha ya Kiebrania; kwa kuwa watu walioko ukutani wanasikiliza.”

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Mungu Mwenyezi, kwako utukufu na heshima! Ee Mungu wangu wa milele, nifundishe kila siku kuzungumza lugha inayopatana na neno lako ili niweze kuwa na lugha ya imani, kwani kupitia hiyo naweza kuwasiliana nawe. Nisaidie kuongozwa na imani yangu ili imani yangu isiwe bubu, bali niweze kuambia mlima uondoke, nao utaondoka, kwani hakika hakuna shida wala hali ipitayo uwezo wako. Bwana, nifundishe kila siku kuwa mbebaji wa utukufu wako kwa wote wanaonizunguka na kila mahali nizungumze lugha ya mbinguni ili niweze kueneza lugha hiyo ya mabadiliko, imani na ushindi. Katika jina la Yesu. Amina!
Tufuate:

Matangazo


Matangazo