Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


91 Mistari ya Biblia kuhusu Kumtumaini Mungu na sio Sanamu

91 Mistari ya Biblia kuhusu Kumtumaini Mungu na sio Sanamu
Zaburi 115:4-8

Miungu yao ni ya fedha na dhahabu; imetengenezwa kwa mikono ya wanadamu. Ina vinywa, lakini haisemi. Ina macho, lakini haioni. Ina masikio, lakini haisikii. Ina pua, lakini hainusi. Ina mikono, lakini haipapasi. Ina miguu, lakini haitembei. Haiwezi kamwe kutoa sauti. Wote wanaoitengeneza wanafanana nayo, kadhalika na wote wanaoitumainia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 62:8

Enyi watu, mtumainieni Mungu daima; mfungulieni Bwana yaliyo moyoni mwenu. Mungu ndiye kimbilio la usalama wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 46:7

Hujitwisha sanamu hiyo mabegani, wakaibeba, kisha huiweka mahali pake, ikakaa papo hapo; kamwe haiwezi hata kusogea kutoka hapo ilipo. Mtu akiililia, haiwezi kumwitikia, wala haiwezi kumwokoa mtu katika taabu zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 118:9

Afadhali kukimbilia usalama kwa Mwenyezi-Mungu, kuliko kuwatumainia viongozi wa dunia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 118:8

Afadhali kukimbilia usalama kwa Mwenyezi-Mungu, kuliko kumtumainia mwanadamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 10:10

Lakini Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa kweli; Mungu aliye hai, mfalme wa milele. Akikasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:5-6

Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 31:6

Wawachukia wanaoabudu sanamu batili; lakini mimi nakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 42:8

Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu; utukufu wangu sitampa mwingine, wala sifa zangu sanamu za miungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 17:5

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Alaaniwe mtu anayemtegemea binadamu, mtu ambaye anategemea nguvu za binadamu, mtu ambaye moyo wake umeniacha mimi Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 26:4

Mtumaini Mwenyezi-Mungu siku zote kwa maana yeye ni mwamba wa usalama milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 10:5

Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndege katika shamba la matango, havina uwezo wa kuongea; ni lazima vibebwe maana haviwezi kutembea. Msiviogope vinyago hivyo, maana haviwezi kudhuru, wala haviwezi kutenda lolote jema.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 146:5-6

Heri mtu anayesaidiwa na Mungu wa Yakobo, mtu aliyeweka tumaini lake kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo. Yeye hushika ahadi yake milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Habakuki 2:18

“Chafaa nini kinyago alichotengeneza mtu? Sanamu ni madini yaliyoyeyushwa, ni kitu cha kueneza udanganyifu! Mtengeneza sanamu hutumaini alichotengeneza mwenyewe, kinyago ambacho hakiwezi hata kusema!

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 40:4

Heri mtu anayemtumainia Mwenyezi-Mungu; mtu asiyejiunga na watu wenye majivuno, watu waliopotoka kwa kuabudu miungu ya uongo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 4:16

Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu mwenye neema, tupokee huruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 41:13

Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ndimi ninayetegemeza mkono wako. Mimi ndimi ninayekuambia: ‘Usiogope, nitakusaidia.’”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 33:22

Fadhili zako zikae nasi, ee Mwenyezi-Mungu, kwani sisi tumekuwekea tumaini letu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 56:11

Namtumainia Mungu, wala siogopi. Binadamu atanifanya nini?

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:14

Mungu asema: “Nitamwokoa yule anipendaye; nitamlinda anayenitambua!

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:31

Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga?

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 39:18

Maana, kweli nitakuokoa na hutauawa vitani; utapata faida ya kuokoa maisha yako kwa sababu umeniamini mimi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 25:1-2

Ee Mwenyezi-Mungu, kwako naielekeza nafsi yangu! Mwenyezi-Mungu hutenda kwa fadhili na uaminifu, kwa wale wanaoshika agano lake na maamuzi yake. Kwa ajili ya jina lako, ee Mwenyezi-Mungu, unisamehe kosa langu kwani ni kubwa. Kila mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu atamfunza njia ya kufuata. Mtu wa namna hiyo atafanikiwa daima, na wazawa wake watamiliki nchi. Mwenyezi-Mungu ni rafiki ya wale wamchao; yeye huwajulisha hao agano lake. Namwangalia Mwenyezi-Mungu daima; yeye atainasua miguu yangu mtegoni. Unielekee, ee Mungu, unionee huruma, maana mimi ni mpweke na mnyonge. Uniondolee mahangaiko ya moyoni mwangu; unitoe katika mashaka yangu. Uangalie mateso yangu na dhiki yangu; unisamehe dhambi zangu zote. Angalia jinsi walivyo wengi maadui zangu; ona jinsi wanavyonichukia kwa ukatili. Nakutumainia wewe, ee Mungu wangu, usiniache niaibike; adui zangu wasifurahie kushindwa kwangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 15:13

Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:26

Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza; atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 57:13

Mtakapolia kuomba msaada, rundo la vinyago vyenu na liwaokoe! Upepo utavipeperushia mbali; naam, pumzi itavitupilia mbali. Lakini watakaokimbilia usalama kwangu, wataimiliki nchi, mlima wangu mtakatifu utakuwa mali yao.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 31:3

Wamisri ni binadamu tu wala si Mungu; farasi wao nao ni wanyama tu, si roho. Mwenyezi-Mungu akiunyosha mkono wake, taifa linalotoa msaada litajikwaa, na lile linalosaidiwa litaanguka; yote mawili yataangamia pamoja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 62:5

Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu; kwake naliweka tumaini langu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 40:31

Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 5:7

Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 94:19

Mahangaiko ya moyo wangu yanapozidi, wewe wanifariji na kunifurahisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 50:10

Nani kati yenu amchaye Mwenyezi-Mungu? Nani anayetii maneno ya mtumishi wake? Kama yupo atembeaye gizani bila taa, amtumainie Mwenyezi-Mungu, na kumtegemea Mungu wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 46:1

Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 3:4-5

Tunaweza kusema hayo kwa sababu ya tumaini letu tulilo nalo kwa Mungu kwa njia ya Kristo. Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:5

Mkabidhi Mwenyezi-Mungu maisha yako; mtumainie yeye naye atafanya kitu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 20:6-7

Najua Mwenyezi-Mungu atamsaidia mfalme aliyemteua, atamjibu kutoka patakatifu pake mbinguni; kwa mkono wake wa kulia atamjalia ushindi mkubwa. Wengine hujigamba kwa magari ya vita; wengine hujigamba kwa farasi wao. Lakini sisi twajivunia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 84:11

Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu; yeye hutuneemesha na kutujalia fahari. Hawanyimi chochote kilicho chema, wale waishio kwa unyofu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 55:6

Mtafuteni Mwenyezi-Mungu wakati bado anapatikana, mwombeni msaada wakati yupo bado karibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:38-39

Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 44:22

Nimeyafagilia mbali makosa yako kama wingu, nimezifanya dhambi zako zitoweke kama ukungu. Rudi kwangu maana mimi nimekukomboa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 33:18

Mwenyezi-Mungu huwaangalia wale wamchao, watu ambao wanatumainia fadhili zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 14:26

Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 145:18

Mwenyezi-Mungu yuko karibu na wote wanaomwomba, wote wanaomwomba kwa moyo mnyofu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 4:18

Palipo na upendo hapana woga; naam, upendo kamili hufukuza woga wote. Basi, mtu mwenye woga hajakamilika bado katika upendo, kwani woga huhusikana na adhabu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 4:8

Nalala na kupata usingizi kwa amani; ee Mwenyezi-Mungu, wewe peke yako waniweka salama.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 1:12

nami nateseka kwa mambo haya kwa sababu hiyo. Lakini niko bado timamu kabisa kwani namjua yule niliyemwamini, tena nina hakika kwamba yeye atakilinda salama kile alichonikabidhi, mpaka siku ile.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 73:26

Hata nikikosa nguvu mwilini na rohoni, wewe, ee Mungu, u mwamba wangu; riziki yangu kuu ni wewe milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:40

Mwenyezi-Mungu huwasaidia na kuwaokoa; huwatoa makuchani mwa waovu na kuwaokoa, maana wanakimbilia usalama kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 26:3

Ee Mungu, wawaweka katika amani walio thabiti, wawaweka katika amani kwa kuwa wanakutegemea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 16:1

Unilinde ee Mungu; maana kwako nakimbilia usalama.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 5:14

Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 1:6

Basi, nina hakika kwamba Mungu aliyeanza kazi hii njema ndani yenu, ataiendeleza mpaka ikamilike katika siku ile ya Kristo Yesu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 56:3

Ee Mungu Mkuu, hofu inaponishika, mimi nakutumainia wewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 28:8

Mwenyezi-Mungu ni nguvu ya watu wake; yeye ni kimbilio la wokovu kwa mfalme wake mteule.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 9:10

Wanaokujua wewe, ee Mungu hukutegemea, wewe Mwenyezi-Mungu huwatupi wakutafutao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 41:10

Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 34:8

Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema. Heri mtu anayekimbilia usalama kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 12:2

Mungu ndiye mwenye kuniokoa, nitamtegemea yeye, wala sitaogopa; Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu; yeye mwenyewe ndiye aniokoaye.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:3

Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kutenda mema, upate kuishi katika nchi na kuwa salama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Nahumu 1:7

Mwenyezi-Mungu ni mwema, yeye ni ngome ya usalama wakati wa taabu. Yeye huwalinda wote wanaokimbilia usalama kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 30:15

Bwana Mungu, Mtakatifu wa Israeli, asema: “Mkinirudia na kutulia mtaokolewa; kwa utulivu na kunitumainia mtapata nguvu.” Lakini nyinyi hamkutaka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 125:1

Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni, ambao hautikisiki bali wabaki imara daima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 31:1

Ole wao wale waendao Misri kuomba msaada, ole wao wanaotegemea farasi, wanaotegemea wingi wa magari yao ya vita, na nguvu za askari wao wapandafarasi, nao hawamtegemei Mtakatifu wa Israeli, wala hawamwombi Mwenyezi-Mungu shauri!

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Samueli 22:31

Anachofanya Mungu hakina dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 45:5

“Mimi ni Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine; hakuna Mungu mwingine ila mimi. Ninakuimarisha ingawa wewe hunijui,

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 29:25

Kuwaogopa watu ni kujitega mwenyewe, lakini anayemtumaini Mwenyezi-Mungu yu salama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 56:4

Namtumainia Mungu na kusifu neno lake; namtumainia Mungu, wala siogopi. Binadamu dhaifu atanifanya nini?

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 27:1

Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu na wokovu wangu, ni nani nitakayemwogopa? Mwenyezi-Mungu ni ngome ya maisha yangu, sitamwogopa mtu yeyote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 44:6

Mwenyezi-Mungu, Mfalme na Mkombozi wa Israeli, naam, Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Mimi ni wa kwanza na wa mwisho; hakuna Mungu mwingine ila mimi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:2

ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu: “Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu; Mungu wangu, ninayekutumainia!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 4:35

Nyinyi mlijaliwa kuyaona mambo hayo, ili mpate kutambua kwamba Mwenyezi-Mungu, ndiye peke yake Mungu na wala hakuna mwingine.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 6:17

Waamuru watu walio matajiri katika mambo ya maisha ya sasa, wasijivune, wasiweke tumaini lao katika mali isiyoweza kutegemewa; bali wamtegemee Mungu, ambaye kwa ukarimu hutupatia vitu vyote tuvifurahie.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 33:21

Naam twafurahi kwa sababu yake; tuna matumaini katika jina lake takatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 43:2

Mkipita katika mafuriko, mimi nitakuwa pamoja nanyi; mkipita katika mito, haitawashinda nguvu. Mkitembea katika moto, hamtaunguzwa; mwali wa moto hautawaunguza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 20:1

Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:4

Atakufunika kwa mabawa yake, utapata usalama kwake; mkono wake utakulinda na kukukinga.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 16:20

Anayezingatia mafundisho atafanikiwa; heri mtu yule anayemtumainia Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 27:3

Hata jeshi likinizunguka, moyo wangu hautaogopa kitu; hata nikikabiliwa na vita, bado nitakuwa na tumaini.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 1:9

Naam, tulikuwa kama watu waliohukumiwa kuuawa, ili tufundishwe kumtegemea Mungu mwenye kuwafufua wafu, badala ya kutegemea nguvu zetu sisi wenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:13

Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 112:7

Hana haja ya kuogopa akipata habari mbaya; ana moyo thabiti na humtegemea Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 23:4

Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:6

Ndiyo maana tunathubutu kusema: “Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 144:2

Yeye ni rafiki yangu amini na ngome yangu, kinga yangu na mkombozi wangu; yeye ni ngao yangu, kwake napata usalama; huyashinda mataifa na kuyaweka chini yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 84:12

Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, heri mtu yule anayekutumainia wewe!

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 45:22

Nigeukieni mimi mpate kuokolewa, popote mlipo duniani. Maana mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 146:3

Msiwategemee wakuu wa dunia; hao ni binadamu tu, hawawezi kuokoa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 62:2

Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu, yeye ni ngome yangu, sitatikisika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 28:7

Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu; tegemeo la moyo wangu limo kwake. Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo; kwa wimbo wangu ninamshukuru.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 18:10

Jina la Mwenyezi-Mungu ni mnara imara; mwadilifu huukimbilia akawa salama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 20:3-4

“Usiwe na miungu mingine ila mimi. “Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago cha chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Tufuate:

Matangazo


Matangazo