Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 9:3 - Swahili Revised Union Version

3 Na Tiro alijijengea ngome, akakusanya fedha kama mchanga, dhahabu safi kama matope ya njia kuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa, umejirundikia fedha kama vumbi, na dhahabu kama takataka barabarani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa, umejirundikia fedha kama vumbi, na dhahabu kama takataka barabarani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa, umejirundikia fedha kama vumbi, na dhahabu kama takataka barabarani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Tiro amejijengea ngome imara, amelundika fedha kama mavumbi, na dhahabu kama taka za mitaani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Tiro amejijengea ngome imara, amelundika fedha kama mavumbi na dhahabu kama taka za mitaani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Na Tiro alijijengea ngome, akakusanya fedha kama mchanga, dhahabu safi kama matope ya njia kuu.

Tazama sura Nakili




Zekaria 9:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

wakaja ngomeni kwa Tiro, na kwa miji yote ya Wahivi, na ya Wakanaani; tena wakaenda katika Negebu ya Yuda huko Beer-sheba.


Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.


Mfalme akafanya fedha humo Yerusalemu kuwa kama mawe, na mierezi akaifinya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.


Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito;


Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi;


Au pamoja na wakuu wenye dhahabu, Waliozijaza nyumba zao fedha;


Amenyosha mkono wake juu ya bahari, amezitikisa falme; Bwana ametoa amri katika habari za Kanaani, kuziangamiza ngome zake.


Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu mataji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia?


Nao wataufanya utajiri wako kuwa mateka, na bidhaa yako kuwa mawindo; nao watazibomoa kuta zako, na kuziharibu nyumba zako zipendezazo; nao watatupa mawe yako, na miti yako, na mavumbi yako, kati ya maji.


Mali zako, na bidhaa yako, na utajiri wako, wanamaji wako, na rubani zako, na wenye kutia kalafati wako, na wafanya biashara wako, na watu wako wa vita wote, walio ndani yako, pamoja na jeshi lako lote lililo ndani yako, wataanguka katika moyo wa bahari katika siku ya kuangamia kwako.


Bidhaa zako zilipotoka katika bahari, uliwajaza watu wa kabila nyingi; uliwatajirisha wafalme wa dunia, kwa wingi wa mali zako, na kwa utajiri wako.


Wakati ulipovunjwa na bahari, katika vilindi vya maji, bidhaa zako na jeshi lako lote walianguka kati yako.


Neno la BWANA likanijia tena, kusema,


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Tiro, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameitia kabila nzima katika mikono ya Edomu, wala hawakulikumbuka agano la udugu;


kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo