Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 8:7 - Swahili Revised Union Version

7 BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na toka nchi ya magharibi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi ya mashariki na kutoka nchi ya magharibi

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi ya mashariki na kutoka nchi ya magharibi

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi ya mashariki na kutoka nchi ya magharibi

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na toka nchi ya magharibi;

Tazama sura Nakili




Zekaria 8:7
21 Marejeleo ya Msalaba  

bali mkinirudia mimi, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, watu wako waliofukuzwa wajapokuwa katika pande za mwisho za mbingu, hata hivyo nitawakusanya kutoka huko, na kuwaleta mpaka mahali pale nilipopachagua ili kuliweka jina langu hapo.


Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la BWANA husifiwa.


BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu, Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.


Mungu, Mungu BWANA, amenena, ameiita nchi, Toka maawio ya jua hadi machweo yake.


Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka magharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu.


Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.


Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwanamke mwenye mimba, na yeye pia aliye na uchungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa.


Basi nena, Bwana MUNGU asema hivi; Nitawakusanya ninyi toka kati ya makabila ya watu, na kuwakutanisha toka nchi zile mlizotawanyika, nami nitawapeni nchi ya Israeli.


Bwana MUNGU asema hivi; Siku ile nitakapowatakaseni kutoka kwa maovu yenu yote, nitaifanya miji ikaliwe na watu, na palipobomolewa pajengwe tena.


Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni BWANA, Mungu wao, nami nitawasikia.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


ndipo BWANA, Mungu wako, atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia BWANA, Mungu wako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo