Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 11:10 - Swahili Revised Union Version

10 Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Nikaichukua ile fimbo yangu niliyoiita “Fadhili,” nikaivunja, kuonesha kwamba agano alilofanya Mwenyezi-Mungu na watu wake limevunjwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Nikaichukua ile fimbo yangu niliyoiita “Fadhili,” nikaivunja, kuonesha kwamba agano alilofanya Mwenyezi-Mungu na watu wake limevunjwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Nikaichukua ile fimbo yangu niliyoiita “Fadhili,” nikaivunja, kuonesha kwamba agano alilofanya Mwenyezi-Mungu na watu wake limevunjwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua agano nililofanya na mataifa yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote.

Tazama sura Nakili




Zekaria 11:10
20 Marejeleo ya Msalaba  

Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri, Mungu ameangaza kote.


Umechukizwa na agano la mtumishi wako, Umelinajisi taji lake na kulitupa chini.


Na fadhili za BWANA, Mungu wetu, ziwe juu yetu, Na kazi ya mikono yetu uifanye thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uifanikishe.


Usituchukie, kwa ajili ya jina lako; usikifedheheshe kiti cha enzi cha utukufu wako, kumbuka, usilivunje agano ulilofanya nasi.


Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga.


Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.


BWANA akasema, Mwite jina lake Lo-ami; kwa maana ninyi si watu wangu, wala mimi sitakuwa Mungu wenu.


Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa. Kisha nikajipatia fimbo mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na ya pili nikaiita, Umoja; nikalilisha kundi lile.


Kwa jumla ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arubaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arubaini, nanyi mtakujua kuchukizwa kwangu.


Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita kabla ya hayo yote kutimia.


Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nilisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau nitawadharau.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo