Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 1:10 - Swahili Revised Union Version

10 Na yule mtu aliyesimama kati ya mihadasi akajibu, akasema, Hawa ndio BWANA aliowatuma, waende huku na huko duniani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Hawa ndio waliotumwa na Mwenyezi-Mungu kuikagua dunia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Hawa ndio waliotumwa na Mwenyezi-Mungu kuikagua dunia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Hawa ndio waliotumwa na Mwenyezi-Mungu kuikagua dunia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewatuma waende duniani kote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambao bwana amewatuma waende duniani kote.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Na yule mtu aliyesimama kati ya mihadasi akajibu, akasema, Hawa ndio BWANA aliowatuma, waende huku na huko duniani.

Tazama sura Nakili




Zekaria 1:10
13 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.


Nao wakamjibu yule malaika wa BWANA aliyesimama kati ya mihadasi, wakasema, Tumekwenda huku na huko duniani, na tazama, dunia yote inatulia, nayo imestarehe.


Niliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya miti ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe.


Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.


Maana yeyote aliyeidharau siku ya mambo madogo watafurahi, naye ataiona timazi ikiwa katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi taa saba ndizo macho ya BWANA; yanaona huku na huko duniani kote.


na tazama, kifuniko cha risasi kiliinuliwa; na tazama, mlikuwa na mwanamke ndani ya kikapu.


Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo