Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 92:4 - Swahili Revised Union Version

4 Kwa kuwa umenifurahisha, BWANA, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Ee Mwenyezi-Mungu, matendo yako yanifurahisha; nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Ee Mwenyezi-Mungu, matendo yako yanifurahisha; nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Ee Mwenyezi-Mungu, matendo yako yanifurahisha; nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ee Mwenyezi Mungu, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ee bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.

Tazama sura Nakili




Zaburi 92:4
20 Marejeleo ya Msalaba  

Utukufu wa BWANA na udumu milele; BWANA na ayafurahie matendo yake.


Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Maana furaha yangu hutoka kwa BWANA.


BWANA alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi.


Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako.


Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.


Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia, Na wote wenye moyo wa adili watasifu.


Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.


Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, Na utukufu wako kwa watoto wao.


Maana BWANA asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee BWANA, uwaokoe watu wako, mabaki ya Israeli.


Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;


Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.


Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.


Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo