Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 57:2 - Swahili Revised Union Version

2 Nitamwita MUNGU Aliye Juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Namlilia Mungu Mkuu, Mungu anikamilishiaye nia yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Namlilia Mungu Mkuu, Mungu anikamilishiaye nia yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Namlilia Mungu Mkuu, Mungu anikamilishiaye nia yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu anayetimiza makusudi yake kwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 57:2
12 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.


Ee BWANA, uniponye kutoka kwa adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche.


Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako;


Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake lipotee?


Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, Maana ni wengi wanaonipiga vita.


BWANA, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.


Njooni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.


Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.


Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;


Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.


awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo