Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 20:1 - Swahili Revised Union Version

1 BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mwenyezi Mungu na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

Tazama sura Nakili




Zaburi 20:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.


Nijapopitia katika shida, Unanilinda juu ya hasira ya adui zangu, Unaunyosha mkono wako, Na mkono wako wa kulia unaniokoa.


BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.


Heri amkumbukaye mnyonge; BWANA atamwokoa siku ya taabu.


Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.


Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.


Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai kitu.


Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.


Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.


Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.


Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.


Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa kutoka kwayo.


Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo