Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 18:3 - Swahili Revised Union Version

3 Namwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa maadui zangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa maadui zangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa maadui zangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Ninamwita Mwenyezi Mungu anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Ninamwita bwana anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Namwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 18:3
26 Marejeleo ya Msalaba  

Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu.


Ndipo Walawi, Yeshua na Kadmieli, na Bani, na Hashabneya, na Sherebia, na Hodia, na Shebania, na Pethahia, wakasema, Simameni, mkamhimidi BWANA, Mungu wenu, tangu milele na hata milele. Na lihimidiwe jina lako tukufu, lililotukuka kuliko baraka zote na sifa zote.


Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Aifundishaye mikono yangu vita, Na vidole vyangu kupigana.


BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hauchunguziki.


Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.


Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu.


Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.


Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Nami nitamwita Mungu, Na BWANA ataniokoa;


Hadi lini mtamshambulia mtu, Mpate kumwua ninyi nyote pamoja? Kama ukuta unaoinama, Kama ua ulio tayari kuanguka,


Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.


Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Ngome imara ya wokovu wangu. Maana wewe, Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.


Wewe U mwenye fahari na adhama, Toka milima ya mateka.


Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;


Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.


Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.


Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.


Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;


Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.


Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo